Waziri wa Michezo atafutia ushirikiano na wawakilishi wa Rolan Garous ya kifaransa


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo alikutana siku ya Alhamisi na wawakilishi wa Rolan Garous inayofuata Shirikisho la Tenisi ya kifaransa katika ofisi yake Wizarani ili kutafutia njia za ushirikiano ya wakati ujao kuhusu kuendeleza na kueneza mchezo wa Tenisi ya Ardhini Nchihi Misri kwa kiwango kikubwa zaidi na hivyo ni Pembezoni mwa ziara ya wawakilishi wa Rolan Garous kwa Misri na kumalizika kwao kwa kujenga klabu ya Rolan Garous ya kimchezo na kijamii mjini mwa Mostakbal uliopo kushoto mwa mji mpya wa kiutawala .


Na mkutano ulijadili njia za ushirikiano kati ya Wizara na shirikisho la Misri la Tenisi na wawakilishi wa Rolan Garous mnamo kipindi kijacho , ambapo walikubaliana na kuanza ushirikiano kwa kutekeleza mashindano ya maonesho kwa ushiriki wa mabingwa wa Tenisi nchini Ufaransa na Misri na kutoa mpango kamili ili kujenga taasisi kwa jina la Rolan Garous ili kueneza mchezo wa Tenisi ya Ardhini Nchi nzima na kueleza ushiriki wa wawakilishi wa Rolan Garous katika mradi wa kitaifa wa talanta na bingwa wa kiolimpiki unaotekelezwa na Wizara ya vijana na michezo kwa kufanya mradi wa kitaifa wa tenisi ya Ardhini.


Na Waziri huyo alieleza vipengele vinavyopambanua Misri kutoka kwa majengo ya vijana na  michezo yanayoenezwa mikoani mwote kupitia vituo vya vijana na klabu za michezo na mlolongo wa klabu ya Klabu unaojumuisha viwanja mahususi vya mchezo wa Tenisi ya Ardhini na alieleza pia mwelekeo wa Wizara wa kuzidisha idadi ya washiriki katika michezo yote kwa uratibu na ushirikiano na mashirikisho tofauti ya kimchezo .


Waziri huyo alikaribisha kwa uwekezaji wa Rolan Garous ya kifaransa Nchini Misri na alisisitiza kujali kwa wahusika wake kwa ushirikiano wenye mafanikio na nchi jirani katika uenezi wa mchezo wa Tenisi ya Ardhini na kufanya miradi mikubwa ya michezo kwa ushiriki wa ndugu kutoka kwa wahusika wa sekta binafsi Nchini falme za kiarabu , akibainisha kwamba Wizara inatoa  misaada yote kwa wawakilishi wa Rolan Garous ili kuimarisha ushirikiano ambapo unafaidisha maendeleo ya michezo ya Misri .


Na waziri wa vijana na michezo  alikubaliana na wawakilishi wa Rolan Garous juu ya kuandaa mkataba ya makubaliano

Unajumuisha vipengele vyote vinavyokubalika vya ushirikiano na kuvitia saini mnamo kipindi kijacho baada ya kumalizika kwa kuvisoma kikamilifu  na pia kuanza kutekeleza maoni ya Rolan Garous ya kueneza mchezo wa Tenisi Nchini Misri na hivyo itasaidia katika uenezi wa mchezo na kuzidisha idadi ya wachezaji wake .


Na kwa upande wao , wawakilishi wa Rolan Garous walieleza furaha yao ya ushirikiano na Misri katika upande wa mchezo na kuanzisha klabu na taasisi za Rolan Garous katika upande wa maendeleo ya mchezo wa Misri na mafanikio mengi ambayo Misri inayashuhudia katika sekta tofauti .


Na kutoka wawakilishi wa Rolan Garous waliohudhuria mkutano :

Bernardibsi , mkuu wa bodi ya  wakurugenzi ya East made Egypt ambaye ni mwakilishi wa Rolan Garous Nchini Misri , Bwana Nicola Doris  mwakilishi wa Rolan Garous huko Paris , Bernard de lasal mkuu wa kundi la odisi la shule za michezo , na Rashed Bin Hidar mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya

Kundi la Bin Hidar la Emirates , Mohammed zahed El batrany ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa kundi la  Bin Hidar na Shokry elnagar Naibu wa Mkuu wa bodi ya wakurugenzi  ya East made Egypt.

Comments