Dokta Ashraf Sobh,
Waziri wa Vijana na Michezo, alishiriki katika tamasha la Mega kwa
pikipiki, Pamoja na ushiriki wa vijana
na wasichana 150 katika tamasha
la baiskeli, ili kukuza na kujiandaa kwa
mwanzo wa Kombe la Mataifa ya kiafrika , Ambapo alianza kutoka Rawd el-Faraj, akipitia uwanja wa Kairo,
kisha Uwanja wa Ulinzi wa ndege , wakiishi kwenye Uwanja wa Amani.
Awamu ya kwanza toka kundi la Mega ilizinduliwa,ambayo
ilifanyika Ijumaa saa nne asubuhi, ama awamu ya pili itazinduliwa katika uwanja
wa Aleskadaria Ijumaa, 21 Juni huu.
Dokta Ashraf Sobhy alisema kuwa tamasha hili linakuja
miongoni mwa maandalizi ya Wizara ya
Vijana na Michezo ili kukuza tukio kubwa la soka ambalo Misri itakuwa na mwezi
mzima, nalo ni Kombe la Mataifa ya kiafrika, ambayo itaanza mnamo tarehe 21 ya
mwezi huu na kumalizika tarehe 19 Julai ijayo, Akielezea kuwa wazo la Mega
linalenga kukuza na kutangaza kwa michuano ya Mataifa ya kiafrika kabla ya
uzinduzi na kuonyesha viwanja vya kushiriki katika njia ya ustaarabu na
kuonyesha vivutio maarufu vya utalii katika mikoa inayoshikilia michuano hayo.
Aliongeza kuwa miongoni mwa
washiriki katika tamasha hili ni mchezaji Abdelrahman Sharif, Shujaa wa
Afrika katika pande tatu na mchezaji Sayed Sharif, shujaa wa Waarabu katika
pande tatu.
Akielezea kwamba wote
ni kutoka mashujaa wa Misri katika michezo mbalimbali daima
hushiriki katika matukio hayo ambayo yanaonyesha jukumu la kijamii kwao, na
aliwashukuru Shirikisho la Baiskeli la kimisri, lililoongozwa na Dokta Wajih Azzam, na Shirikisho la kimisri la
Triathlon lililoongozwa na Jenerali Mkuu Ahmed Nasser.
Tamasha hilo limetekelezwa kwa Idara kuu ya Maendeleo ya
kimichezo katika Wizara ya Vijana na Michezo, iliyoongozwa na Jenerali Ismail Al-Far, kwa kushirikiana na Uongozi wa
Vijana na Michezo, iliyoongozwa na Dokta
Ashraf Al-Bajrami.
Comments