Waziri wa Michezo aonesha Jaribio la Misri katika kukabiliana na Janga la Corona katika nyanja mbili za Vijana na Michezo, hilo katika Mkutano wa Mawaziri wa Masuala ya Kijamii nchini Saudi Arabia

Waziri wa Vijana na Michezo, Dokta.Ashraf Sobhy, alishirikiana na Mkuu wa Ofisi ya Utendaji wa Baraza la Mawaziri waarabu wa Vijana na  Michezo, Jumanne  katika shughuli za Mkutano wa Mawaziri wa Masuala ya Kijamii na Mabaraza ya Wizara za kiarabu  yanayohusika na sekta za kijamii, na Jukwaa la Mpango wa Usimamizi wa Mabadiliko ya Kijamii (MOST) kwa Mawaziri waarabu wa Masuala ya Kijamii chini ya kichwa "matokeoTofauti ya Janga la Corona (COVID-19) "Kutengeneza njia za kupata nafuu  kwa eneo la Kiarabu na kusaidia vikundi vilivyo hatarini na dhaifu katika maradhi  na migogoro"


Mkutano huo utafanyika mjini Riyadh,  nchini Ufalme wa Saudi Arabia, kwa Mahudhurio ya Mhandisi. Ahmed bin Suleiman Al-Rajhi, Waziri wa Rasilimali  za binadamu  na Maendeleo ya Jamii katika Ufalme wa Saudi Arabia, Mheshimiwa  Ayman Al-Mufleh, Waziri wa Maendeleo ya Jamii katika Ufalme wa Hashemite wa Jordan, Mkuu wa Ofisi ya Utendaji ya Baraza la Mawaziri wa Masuala ya Jamii, na Balozi Dokta. Haifa Abu Ghazaleh, Katibu Mkuu Msaidizi wa Umoja wa Nchi za Kiarabu, Mkuu wa Sekta ya Masuala ya Kijamii, Gabriela Ramos, Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Sayansi ya Kijamii na Kibinadamu kwenye UNESCO, na kundi la Waheshimiwa na Wakuu Mawaziri waarabu wa Masuala ya Kijamii, na Mawaziri wanachama wa Ofisi za Utendaji za Mabaraza ya Wizara za Kiarabu.


Waziri wa Vijana na Michezo alianza kauli yake kwa kuelezea salamu za Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, na matumaini yake ya kufanikisha mkutano  muhimu huo , akielezea furaha yake ya kushirikisha katika shughuli  za mkutano huo

Comments