Jukwaa hilo linazingatiwa kama jukwaa muhimu lililotenganezwa na vijana , ili kupeleka ujumbe wa Amani na Ustawi na Ushirikiano , lilitolewa kwa Dunia nzima , ambapo vijana wa Duniani kote hushiriki katika sherehe muhimu ya kimataifa na yenye kiwango cha juu , ili kuonesha maoni yao na kuwa na ushauri na mikutano mingine , pamoja na Mahudhurio ya viongozi wa Dunia na wahusika maarufu , kwani mkutano ni fursa ya kuwasiliana na wahusika wakubwa wenye maamuzi muhimu pamoja na wanafikra nzuri kuhusu Dunia, pia ni fursa ili kufahamu vijana wengi wa uraia mbalimbali ulimwenguni , vijana ambao wana ndoto pia utashi na wanataka kufanya mabadiliko halisi katika Dunia ya leo na kesho .
Uzinduzi wa kwanza wa jukwaa hilo :
Tarehe 25 Aprili 2017 , baadhi ya vijana wamisri , kwenye mkutano wa kitaifa wa vijana mkoani Asmalia , walitoa fikra zao za kuanzisha mahojiano na vijana Duniani , Mheshimiwa Rais Abd El-Fatah El Sisi akatangaza mwaliko wake kwa vijana wote kutoka nchi mbalimbali , ili kuonesha maoni yao na mitazamo yao ya mustakabali wa nchi zao na Dunia nzima .
Jukwaa lilifanyika kwa mara ha kwanza mnamo Novemba 2017 , na tangu muda huo , furasa ikawa wazi kwa vijana ili kuwasiliana na watoa maamuzi wakuu , na kuwasiliana pamoja na vijana wenye mustakabali mzuri Barani na Duniani kote , wakitaka kuufanya Dunia mahali pema kwa wote .
Jukwaani , watu mbalimbali walishiriki , ikijumuisha marais wa nchi na serekali , viongozi vijana wa kimataifa , vijana wenye mawazo katika nyanja tofauti , na watu mashuhuri wa kimataifa na vikundi vya vijana kutoka Duniani kote .
Toleo la nne la Jukwaa :
Litazinduliwa toleo la nne la jukwaa kati ya kipindi 10 mpaka 13 Januari ,2022 , mkoani Sharm El Sheikh kusini mwa Sinai chini ya usimamizi wa Rais Abd El Fattah El Sisi , usajili umefunguliwa kwa vijana wanaotaka kuhudhuria shughuli za Jukwaa nchini Misri na kutoka nchi zote za ulimwengu tokea siku ya Jumatatu tarehe 15 Novemba 2021 mpaka 15 Desemba .
Pointi muhimu za Jukwaa :
Jukwaa linajumuisha maudhui tatu muhimu :( Amani , Maendeleo na Ubunifu ), kupitia kwake maudhui nyingi zinazohusu vijana hujadiliwa, linalounda Jukwaa la kubainisha mitazamo ya maoni na kutoa mawazo, kubadilishana na uzoefu kupitia kwa vikao na Semina
Comments