Mawaziri wawili wa Awqaf na Vijana wajadili njia za kuimarisha mawasiliano na vijana
- 2022-01-06 22:48:12
Sobhy:
Ushirikiano usio na kifani pamoja na Wizara ya Awqaf
Tunathamini jukumu lake katika kujenga maelewano kati ya vijana:
Jumaa:
Kuimarisha mawasiliano na vijana ni mojawapo ya vipaumbele vyetu muhimu zaidi mnamo 2022
Na kazi ya pamoja kati ya taasisi za nchi inashuhudia mabadiliko makubwa ya ubora ili kufikia maslahi ya kitaifa
Na tunahitaji juhudi za kuendelea ili kuenda kutoka utamaduni wa wasomi kuelekea utamaduni wa jamii.
katika mfumo wa ushirikiano unaoendelea na wenye tija kati ya Wizara ya Awqaf na Wizara ya Vijana na Michezo, Mheshimiwa Prof. Muhammad Mukhtar Jumaa, Waziri wa Awqaf, amempokea Mheshimiwa Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo katika makao makuu ya Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu,Jumatatu tarehe 3/1/2022 ili kujadili njia za ushirikiano wa pamoja kati ya wizara hizo mbili.
wakati wa mkutano huo, Mheshimiwa Prof. Dkt. Muhammad Mukhtar Jumaa, Waziri wa Awqaf, alisisitiza kwamba kazi hiyo ya pamoja kati ya taasisi za serikali inazingatiwa kuwa mabadiliko ya ubora katika kazi ya kundi la pamoja, na tunahitaji jitihada za kuendelea ili kwenda kutoka utamaduni wa wasomi kwa utamaduni wa jamii, na pia alisisitiza kuwa kuongeza mawasiliano pamoja na vijana ni moja ya vipaumbele vyetu muhimu zaidi mnamo 2022, na katika mfumo wa kujenga uelewano baina ya vijana, darzeni 500 za vitabu vya maoni ya Mawazo yaliyoelimika, toleo la pili, zilitolewa kwa Wizara ya Vijana na Michezo ili zigawanyike kwa vituo vya vijana na klabu za michezo.
Kwa upande wake Mheshimiwa Prof.Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo alisisitiza kuwa Wizara ya Awqaf inafanya juu chini ili kuujenga uelewano na kuueneza kati ya vijana kupitia machapisho yake mashuhuri, semina na makongamano ya kisayansi kwa ushirikiano na Awqaf. kupitia maimamu wake ili kushirikisha katika kozi za mafunzo zinazofanywa kwa Wizara ya Vijana na Michezo.
Mheshimiwa Prof. Muhammad Mukhtar Jumaa, Waziri wa Awqaf, alimpa Mheshimiwa Prof. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo nakala ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu (Kurani Tukufu) na darzeni ya pili ya machapisho ya vitabu vya "Maoni" kwa mawazo yaliyoelimika, na darzeni ya machapisho mapya zaidi ya Wizara ya Awqaf na Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu
Comments