Ashraf sobhy apongeza bodi mpya Ya wakurugenzi ya Shirikisho la mpira la Misri

Dokta Ashraf sobhy : natamani  mafanikio yote kwa bodi mpya ya wakurugenzi ya Shirikisho la Misri na tunasubiri mafanikio zaidi mnamo kipindi kijacho .. na kuna sherehe ya kuwaheshimu wanachama wa kamati ya pande tatu na kamati ya pande tano kwa ajili ya mchango wao thabiti katika Shirikisho mnamo kipindi kilichopita .


Waziri wa Vijana na Michezo Dokta Ashraf Sobhy alipongeza bodi mpya

ya wakurugenzi ya Shirikisho la Misri la mpira wa miguu kwa uongozi wa Gamal Allam baada ya kushinda katika uchaguzi uliofanyika  , akitamani mafanikio kwa bodi ya wakurugenzi mnamo kipindi kijacho ambapo itasaidia katika kuendeleza mpira wa miguu wa Misri na kuhakikisha mafanikio zaidi kwake .


Na pia Dokta Ashraf Sobhy alitoa pongezi na Shukurani kwa kamati ya pande tatu kwa uongozi wa Mhandisi Ahmed Megahed na pande tano kwa uongozi wa Amr Elganaini kwa ajili ya Usimamizi wao wa hekima ya Shirikisho la mpira katika kipindi kilichopita na kuhifadhi  Utulivu wa mfumo wa mpira wa Misri na pia kufanya mashindano tofauti ya Shirikisho kwa utaratibu .


Waziri huyo alitangaza kufanyika sherehe ya kuwaheshimu  wanachama wa kamati mbili mnamo kipindi kijacho

Kulingana na jukumu lao thabiti 

Katika Usimamizi wa Shirikisho la mpira kipindi kilichopita kwa kuhudhuria bodi mpya ya wakurugenzi ya Shirikisho .


Na orodha ya kwanza  kwa uongozi wa Gamal Allam imeshinda uchaguzi wa bodi ya wakurugenzi ya Shirikisho la Misri la mpira wa miguu uliofanyika wakati wa mkutano wa baraza kuu la Shirikisho , na orodha inajumuisha  Gamal Allam  kama Mkuu, Khaled Eldrandly kama Naibu wa Mkuu na wanachama Mohamed Helmy Mashhour , Mohammed Abu Elwafa , Hazem Imam , Mohammed Barakat , Ihab Elkomy , Amer Hussien na Dina Elrefaii

Comments