"Amani, Ubunifu na Maendeleo" .. Ajenda ya Kongamano La Nne La Vijana Duniani

 Kongamano la Vijana Duniani litafanyika kuanzia Januari 10 hadi 13, 2022 huko Sharm El Sheikh, Sinai Kusini, chini ya uangalizi na kuwepo kwa Rais Abd El-Fatah El Sisi.

 

Wasimamizi wa kongamano hilo walitangaza ajenda ya toleo la nne,  linalojumuisha masuala kadhaa muhimu na mada zinazoakisi sifa za hali halisi  mpya baada ya Janga la Corona (Covid-19),  lililoathiri maisha ya mamilioni ya watu Duniani kote.


Mada zote zinatokana na mada kuu tatu za kongamano hilo nazo ni “Amani, Ubunifu na Maendeleo”.


Kabla ya uzinduzi wa kongamano hilo, warsha kadhaa za maandalizi zilifanyika kwa muda wa siku mbili kujadili athari za Janga la Corona kwa kuzingatia nyanja mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mapitio ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa 2030, mustakabali wa Bara la Afrika, mustakabali wa teknolojia ya kifedha kwa masoko yanayoibukia, mabadiliko ya kidijitali, elimu, na mtazamo wa kizazi cha vijana Duniani baada ya Janga hilo.


Pamoja na kuangalia maswala muhimu ambayo ni pamoja na kupitisha sera za busara za maji, kushughulikia changamoto za mazingira, na jukumu linalokua la kimataifa kwa Kampuni zinazoanza.  Mbali na kupitia upya mpango wa "Maisha yenye Heshima" kama uzoefu wa Misri kwa maendeleo ya binadamu.


Kongamano la Vijana Duniani litaanza Jumatatu, Januari 10, kwa sherehe za ufunguzi, na kufuatiwa na kikao cha mawasilisho kuhusu Janga la Corona kama onyo na matumaini mapya kwa Utu


Na mnamo siku mbili zijazo, vikao kadhaa, warsha na matukio yatafanyika ili kujadili masuala kadhaa muhimu, ikiwa ni pamoja na njia za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kutoka Glasgow hadi Sharm El Sheikh, mustakabali wa huduma za afya na athari za kitabia na kisaikolojia wakati baada ya Janga hilo, pamoja na kuonesha uzoefu wa maendeleo katika kukabiliana na Umaskini.


Ajenda ya kongamano hilo pia inatoa masuala mengine mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vikao vya majadiliano juu ya mustakabali wa nishati, usalama endelevu wa maji, amani na usalama wa kimataifa, ujenzi wa maeneo baada ya migogoro.kongamano hilo pia linalenga kuzingatia maadili ya binadamu kwa kujadili sanaa na ubunifu, na kujenga ulimwengu salama na kikamilifu kwa wanawake.


Kwa kuzingatia shauku ya kongamano la Vijana Duniani tangu kuanzishwa kwake katika kuandaa mifumo ya kuiga, mwaka huu modeli ya uigaji ya Umoja wa Mataifa itafanyika kwa Baraza la Haki za Kibinadamu.


Shughuli zilizoanzishwa na kongamano katika miaka iliyopita pia zitaendelea kupitia Jumba la Michezo la Vijana Duniani, Freedom.e, Inspire.D, na Start Vein.


Aidha, kongamano linazindua matukio kadhaa mapya maalum  yanayowasilishwa kwa mara ya kwanza mwaka huu

Comments