Ashraf Sobhy akutana na Waziri wa Nchi anayeshughulikia Masuala ya Vijana katika UAE .. na watangaza kanuni za ushirikiano kati ya Wizara na Kituo cha Vijana waarabu
- 2022-01-12 23:41:44
Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo na Mkuu wa Ofisi ya Utendaji ya Baraza la mawaziri wa Vijana na michezo ya kiarabu alikutana na Mheshimiwa Shamma Al Mazrouei, Waziri wa Nchi wa Masuala ya Vijana Huko UAE na Makamu wa mkuu wa kituo cha Vijana waarabu. na hilo mnamo Jumatatu, tarehe 10 Januari , 2022 na hivyo imekuwa pembeni mwa ushiriki wake kama mzungumzaji katika kikao kikuu cha kongamano la Vijana Duniani "Janga la Corona ... onyo kwa Utu na tumaini jipya," kwa mahudhurio ya Mheshimiwa Rais. Abd El Fatah El-Sisi.
Waziri wa Vijana na Michezo alimkaribisha Mheshimiwa Shamma Al Mazrouei, akisifu juhudi zake katika kuimarisha na kuendeleza uwezo wa vijana wa UAE.
Mkutano huo ulijadili programu za pamoja zinazoweza kutekelezwa katika nchi hizo mbili ili kuendeleza na kujenga uwezo wa vijana, wakisifu mahusiano ya pande mbili yanayounganisha Jamhuri ya Kiarabu ya Misri na nchi ya UAE.
Mkutano huo pia ulishughulikia jinsi ya kutekeleza na kuamsha ushirikiano wa nchi mbili katika Kiwango cha vijana pamoja na kutangaza kanuni za ushirikiano zinazotarajiwa kati ya Wizara ya Vijana na Michezo ya Misri na Kituo cha Vijana waarabu , kwa kuzingatia mahusiano thabiti ya nchi mbili na ushirikiano wa pamoja, na kuwahi umuhimu wa kuhudumia sekta ya vijana, ushiriki hai wa vijana waarabu
na kutekeleza mipango ambayo itakidhi mahitaji na huduma kwa vijana waarabu
Comments