Dokta Ashraf Sobhy akutana na mjumbe wa Umoja wa Afrika kwa vijana wakati wa ushiriki wake katika kongamano la vijana Duniani
- 2022-01-13 18:47:27
"Sobhy" : vijana waafrika ni Msingi kwa maendeleo ya bara na mhimili mkuu katika Ajenda ya Afrika 2063 ... na wizara ina kamati maalum ya masuala ya kiafrika ili kuunga mkono Ushirikiano wa kiafrika .
Mjumbe wa Umoja wa kiafrika kwa vijana : ziara yangu ni ya kwanza nchini Misri ... Nami nampongeza Rais Abd El Fatah El Sisi kwa mafanikio ya kongamano la vijana Duniani .
"Shedo": tunaomba kuongeza Ushirikiano na vijana wamisri ... na kukuza mipango ya kujitolea barani Afrika .
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo alikutana na Bi. Shedo Kilopatra Mbemba, Mjumbe wa Umoja wa Afrika kwa vijana , hiyo pempezoni mwa mahudhurio yake katika kongamano la vijana Duniani katika toleo lake la nne kwa kuhudhuria kwa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El Sisi .
Dokta Ashraf Sobhy alimkaribisha Mjumbe wa Umoja wa Afrika kwa vijana, akielezea Furaha yake kwa ziara yake nchini Misri na Ushiriki wake katika Jukwaa la Vijana Duniani.
Dokta Ashraf Sobhy alisema :" vijana waafrika Wana matatajio makubwa kwa miaka ijayo , na pia wao ni Msingi katika maendeleo ya bara la Afrika , na mhimili mkuu katika Ajenda ya Umoja wa Afrika 2063,nayo ni Ajenda nzuri mno inatambua kwamba kuwezesha vijana kunachangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya Afrika ".
Comments