Waziri wa michezo ahudhuria sherehe ya kura ya kombe la Dunia la Klabu za mpira wa kikapu

Jumamosi, Januari 15, huko Eneo la Panorama ya Piramidi,Waziri wa vijana na michezo Dokta Ashraf Sobhy alihudhuria Sherehe ya Kura ya  mashindano  ya kombe la Dunia la Klabu za mpira wa kikapu yatakayokaribishwa hapa nchini Misri, Februari ijayo kama  Muonekano wa Kwanza wa mashindano barani Afrika .


Shughuli za sherehe ya kura zilihudhuriwa na Mkuu wa Shirikisho la Misri la mpira wa kikapu Dokta Magdy Abo Frikha , Naibu wa Mkuu wa Shirikisho la Afrika la mpira wa kikapu na Mkuu wa eneo la tano la kiafrika Hisham Elhariri , Mwakilishi wa Shirikisho la kimataifa la mpira wa kikapu "FIBA" Patrick komininos , wawakilishi wa timu zinazoshiriki katika mashindano na Nyota wa timu ya kitaifa ya Misri na nyota wa zamani wa klabu ya zamalek 

Kocha Ahmed Hossam Mido ndiye aliyesimamia kura Mashindano yatafanyika katika sebule ya Dokta h

Hassan Mostafa huko mjini 6 Oktoba , kwa ushiriki wa klabu ya zamalek bingwa wa Afrika , klabu ya Borgos ya Uhispania  ikiwakilisha Ulaya , klabu ya Flamingo ya Brazil ikiwakilisha  Marekani ya kusini  na klabu ya lik land magic ya Marekani bingwa wa G-league na mwakilishi wa NBA 


Katika kauli yake , Dokta Ashraf Sobhy alilisifu Shirikisho hilo ni Shirikisho lenye Ushirikiano wa kimataifa , lengo lake ni kufanya kazi kwa maslahi ya nchi , akiashiria juhudi za Shirikisho la kuendeleza mpira wa kikapu wa Misri , kuwepo kwa ligi nguvu pamoja na kujali juhudi za kukaribisha kwa Misri kwa mashindano ya kombe la Dunia la Klabu la mpira wa kikapu kwa mara ya kwanza Barani Afrika.


Na Waziri huyo aliendelea akisema kwamba kukaribisha Misri kwa 

Mashindano hayo ni mwendelezo wa njia ya Misri ya kukaribisha matukio na mashindano ya michezo ya kimataifa kwa msaada kamili wa uongozi wa kisiasa wa Misri ikiongozwa na Rais wa Jamhuri, Mheshimiwa Abd El-Fatah El Sisi , akiashiria

Kutoa misaada yote kwa mashirikisho tofauti ya kimichezo ya kimisri ili kutekeleza programu na mipango yote na kushirikiana na mashirikisho ya kimataifa kuhusu kukaribisha Misri kwa mashindano yake tofauti .


Kutoka upande wake , Dokta Magdy Abu Frikha aliwakaribisha waliohudhuria sherehe ya kura na alishukuru  Shirikisho la kimataifa la mpira wa kikapu kwa kufanya mashindano nchini Misri , akisifu mchango wa Waziri wa vijana na michezo na misaada yake ya kudumu kwa mashirikisho yote .


Na Hisham Elhariri alisema : " tunaishi Wakati wa kihistoria kwa kufanya kombe la Dunia la Klabu za mpira wa kikapu kwa mara ya kwanza nchini Misri na kwa Ushirikiano wa kimisri kwa timu ya klabu ya Zamalek " akishukuru Shirikisho la kimataifa kutoa nafasi hiyo kwa Misri

 kukaribisha mashindano  na misaada kamili ya Waziri wa vijana na michezo kukaribisha kwa misri kwa mashindano tofauti ya kimataifa .


Wakati ambapo Mwakilishi wa Shirikisho la kimataifa la mpira wa kikapu alisisitiza imani yake katika uwezo wa Misri katika kupanga na kukaribisha mashindano kwa kiwango cha juu , akiashiria Ushirikiano wa ufanisi wa mashirikisho ya kimisri na ya kiafrika Katika harakati za kupata mashindano bora zaidi

Comments