Waziri wa Vijana na Michezo ashuhudia uzinduzi wa Chuo cha Kiafrika cha Tiba ya kimichezo
- 2022-01-19 16:50:50
Sobhi: Chuo cha Kiafrika cha Tiba ya Michezo ni hatua muhimu ya mabadiliko katika kubadilisha hali halisi ya matibabu ya michezo nchini Misri, na kugeuza Kairo kuwa kituo cha mafanikio kuelekea maendeleo ya dawa za michezo Barani Afrika.
Waziri wa Vijana na Michezo Dokta Ashraf Sobhi alishuhudia mkutano wa waandishi wa habari wa uzinduzi wa Chuo cha Kiafrika cha Tiba ya kimichezo na Sayansi za Michezo kilichopo nchini Misri na kinahusishwa na Shirikisho la Madawa ya Michezo Afrika linaloongozwa na Daktari Constant Antoine Roux kutoka Côte d 'Ivoire.
Wakati wa hotuba yake, DKT. Ashraf Sobhi alisema: "Wakati umewadia kuzingatia sana dawa za michezo nchini Misri, kwani Chuo cha Tiba cha Kiafrika kitatumika kama hatua madhubuti ya kubadilisha uhalisia wa tiba ya michezo nchini Misri. ngazi za juu, na kuugeuza Kairo kuwa kituo chenye mafanikio na chenye ushawishi mkubwa kwa maendeleo ya dawa za michezo Barani Afrika".
Waziri huyo aliongeza: "Suala la dawa za michezo ni moja ya faili muhimu sana ambazo Wizara ya Vijana na Michezo inafanyia kazi ili kuendeleza nchini Misri kwa mawazo tofauti kwa ngazi zote, na kufanya kila juhudi kutekeleza ujumbe uliokabidhiwa kwake kikamilifu," akibainisha kuwa Misri inakaribia kuwa mwenyeji wa Mkuu wa Shirika la Dunia la Vichocheo. Ziara yake ni ya kwanza ya aina yake nchini Misri, ikisisitiza jukumu muhimu na kuu la Misri Barani Afrika.
Kwa upande wake, Mkuu wa Shirikisho la Madawa ya Michezo Afrika, katika hotuba yake aliyoitoa kwa niaba yake na Mjumbe wa Ofisi ya Utendaji ya Shirikisho hilo, Reham Raouf, alisema: “Kuna umuhimu wa kuanzisha Chuo cha Tiba ya Michezo, na napenda kuishukuru Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kwa kuanzisha Chuo hicho na kuwa cha kwanza barani Afrika kinachohusisha katika masuala ya dawa za michezo na sayansi za michezo.Napenda kumshukuru Waziri wa Vijana na Michezo wa Misri kwa msaada wake kwa Mashirikisho ya Afrika.
Kwa upande wake, Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Vichocheo nchini Misri (NADO) na Mkurugenzi wa Hospitali ya Nile Valley, Dokta.Hazem Khamis amethibitisha kuwa dawa za michezo zimekuwa na umuhimu mkubwa katika mfumo wa kimataifa wa dawa, na kupongeza jukumu linalotolewa na chuo hicho, ambayo ni ya kwanza ya aina yake Barani Afrika, na shukrani kwa DKT. Ashraf Sobhi, Waziri wa Vijana na Michezo kwa msaada wake kamili wa dawa za michezo nchini Misri kupitia msaada wake wa kuanzishwa kwa Chuo hicho.
Meja Jenerali Ahmed Nasser, Mkuu wa Shirikisho la Mashirikisho ya Afrika "OXA", alieleza fahari yake kwamba Misri ni uzinduzi wa kwanza wa Chuo cha Madaktari wa Michezo barani Afrika, ambao ni ushahidi bora wa nafasi ya Misri ndani ya bara la Afrika.
Kwa upande wake, DKT. Naima Al-Qasir, Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani, alisifu uzoefu wa Misri katika kukabiliana na Janga la Corona, na pia alipongeza wazo la kuanzishwa kwa Chuo cha Madawa ya Michezo cha Kiafrika chenye makao makuu yake nchini Misri, akisisitiza haja ya kufikia maadili ya dawa ya Michezo na kufikia Udijiti wa Afya.
Katika hotuba yake Mkuu wa Idara Kuu ya Tiba ya Michezo Wizara ya Vijana na Michezo na Katibu Mkuu wa Chuo hicho Dokta .Khaled Masoud alipitia muhtasari wa dawa za michezo na uanzishaji wake pamoja na dira, dhamira na kanuni muhimu zaidi za jumla za kuanzisha Chuo na lengo la kuanzishwa kwake, pamoja na mitaala ya mafunzo na programu zinazopendekezwa ndani ya Chuo
Comments