Mafanikio mapya.. Waziri wa Michezo aipongeza timu ya Paralympic kwa kutwaa Ubingwa wa Afrika kwa Mpira wa Kikapu
- 2022-02-01 13:59:43
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, aliupongeza ujumbe wa timu ya Paralympic ya Misri (Ulemavu) kwa mpira wa kikapu juu ya viti vya magurudumu, baada ya kushinda taji la michuano ya Afrika, iliyofanyika nchini Ethiopia ndani ya kipindi cha 20 hadi 30 Januari 2022.
Timu ya kitaifa iliweza kuishinda timu ya Afrika Kusini katika Fainali ya michuano ya Afrika, 60-58, na kwa ushindi huo, timu ya mpira wa kikapu ya Paralympic inafikia Mashindano ya Dunia ya UAE 2022, baada ya kutoshiriki katika michuano hiyo ya kimataifa tangu 1998.
Waziri huyo aliusifu utendaji wa wachezaji wa timu ya kitaifa ya Misri wenye Ulemavu, na kucheza kuzuri kwao katika michuano ya mpira wa kikapu ya Afrika na kuweza kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kwa hatua zake mbalimbali,wakishinda Fainali ya michuano hiyo, na kushinda taji lake, katika mafanikio mapya yanayoongezwa kwa michezo ya Misri mnamo 2022.
Waziri alitilia maanani kwa kuratibu na Kamati ya Paralympic ili kuandaa sherehe kubwa kwa wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya Paralympic; kuthamini mafanikio yao ya michezo, na kuwahimiza waendelee kwa kuzingatia na kufanya mazoezi kwa bidii Katika kujiandaa kwa Mashindano ya Dunia huko UAE, yanayotarajiwa kuzinduliwa Novemba mwaka huu, akisisitiza imani yake katika uwezo wa wachezaji wa kiume na wa kike wa
Misri wa kutoa utendaji na maonyesho ya nguvu na maonyesho bora mwafaka na michezo ya Misri katika majukwaa mbalimbali ya kimataifa
Comments