Waziri wa Vijana akutana na Rais wa Baraza la Uchumi la Afrika


Dokta Ashraf Sobhy Waziri wa Vijana na Michezo alikutana na Balozi Mohamed Abdel Ghaffar Rais wa Baraza la Uchumi la Afrika ili Kujadili njia za kuimarisha ushirikiano wa pamoja.


Waziri wa Vijana na Michezo alisisitiza kuangalia maoni na matarajio yanayopelekea kuimarisha uhusiano wa Misri na Afrika kupitia michezo kama nguvu zenye ushawishi katika kuendeleza mahusiano na nchi za Afrika kwa ushirikiano na uratibu na Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri.


Akiashiria kuwa Wizara ina nia ya kuunga mkono ushirikiano wa pamoja na nchi zote za Bara la Afrika katika nyanja mbalimbali za vijana na kuongeza ushiriki wa vijana wetu waafrika katika shughuli , miradi na programu nyingi zinazotekelezwa na Wizara hiyo haswa katika masuala ya mafunzo na kuwezesha .


Kwa upande wake, Balozi Mohamed Abdel Ghaffar alieleza kuwa Misri inaunga mkono na ni mhusika wa miradi ya nchi za Afrika na inazidisha mifumo ya usaidizi wake , akieleza kuwa Baraza hilo linafanya kazi kwa kushirikiana kwa kiasi kikubwa na Wizara ya Vijana na Michezo.


Bwana Maged Abu al-Khair, mkuu wa Kamati ya Afrika katika Wizara ya Vijana na Michezo alisema kuwa kufanya kazi katika masuala ya Afrika kunahitaji mawazo na tafiti zinazohusiana na mafaili mengi, pamoja na kuunganisha mawazo na kubainisha maono ili kutayarisha

 vielelezo vya kazi vinavyofaa kwa maendeleo ya Bara la Afrika na kutatua masuala yake kupitia kazi ya  ushirikiano wa pamoja kati ya Wizara ya Vijana na Michezo na mamlaka mbalimbali zinazohusika.

Comments