"Mimi ni Mmisri ... Mimi ni Mwafrika." .. Afromedia yazindua programu ya kitaifa " Mimi ni Mmisri.... Mimi ni Mwafrika" ili kuwajenga kada za wanafunzi katika masuala ya kiafrika

Mpango wa Afromedia ulianza vikao vyake vya kwanza ndani ya  programu ya kitaifa "Mimi ni Mmisri ... Mimi ni Mwafrika" ili kuwafundisha  kada za wanafunzi katika masuala ya kiafrika, ambayo imeandaliwa na mpango wa Afromedia  kwa ushirikiano na Taasisi ya Afrika ya Maendeleo na kuimarisha Uwezo, Baraza Huru la Ushauri la Vijana kwa Mkataba wa Biashara Huria barani Afrika, na Umoja wa Wanafunzi wa Afrika .Pamoja na mhadhara wenye mada ya “Utangulizi wa Uchumi wa Afrika”, uliowasilishwa na Dokta. Samar Al Bagoury - Profesa Msaidizi wa Uchumi, Kitivo cha Mafunzo ya Juu ya Afrika, Chuo Kikuu cha Kairo, kama kipindi cha kwanza cha programu hiyo ambacho kilifanyika kwa siku mbili, Februari 4 na 5, 2022, na shughuli za programu hiyo zimepangwa kuendelea hadi Jumamosi Februari 12, kwa Ushirikiano wa kundi la viongozi na vyama vya wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali vya Misri.


Mwanzoni mwa mazungumzo, Hassan Ghazaly, mwanzilishi wa mpango wa Afromedia , alizungumzia  wazo la programu , lililokuja kulingana na  jukumu la kihistoria la harakati za wanafunzi barani Afrika katika enzi za ukombozi wa Waafrika na harakati za kitaifa. mapambano yake dhidi ya ukoloni na athari zake kubwa katika kukomesha  ubaguzi wa rangi, akiashiria Umuhimu wa  kuwashirikisha viongozi wa vyama vya wafanyakazi, katika jukumu lililokabidhiwa kwa michakato ya maendeleo ya kiutamaduni na  jamii zao, mazingira yao ya ushawishi, na kuwawezesha kutekeleza jukumu lao katika kuelimisha wenzao na kuimarisha ujuzi na utaalamu wao, haswa katika nyanja za mambo ya kiafrika. 


Katika muktadha unaohusiana, Imlot Allan David, Rais wa Baraza Huru la Ushauri la Vijana la Bara katika Kanda ya Afrika ya Kati, alisisitiza kwamba mchakato wa kuhamasisha vijana, haswa katika vyuo vikuu kupitia vyama vya wanafunzi, kuzunguka Mkataba wa Biashara Huria wa Afrika ni muhimu sana, akiashiria. kwamba hiyo itachangia katika Kuwawezesha vijana kushiriki na kunufaika na Mkataba wa Biashara Huria Barani Afrika, fursa na juhudi zao kwa muda mrefu zitaongeza tija, na hivyo kuongeza kipato, Ambayo inachangia kumaliza  umaskini  Barani Afrika, na ni jukumu letu muhimu zaidi kama vijana katika kipindi cha sasa. 


Kwa upande wake, Al-Bagoury alisifu wazo la programu ya kitaifa "Mimi ni Mmisri ... Mimi ni Mwafrika," akisisitiza kwamba vyama vya wanafunzi vinaweza kupiga hatua ya kweli katika uelewa wa pamoja miongoni mwa vijana katika vyuo vikuu iwapo watatekeleza wajibu wake katika kuongeza uelewa, kuhamasisha na kuelimisha kuhusu kutambulisha bara la Afrika, haswa kuhusu matarajio ya Ajenda ya Afrika 2063, na kuimarisha uelewa kuhusu Mkataba wa Eneo Huria la Biashara la Afrika, kuzingatia misingi hii miwili ndiyo njia ya kuelekea Afrika tunayoitaka. 


Katika muda wa siku mbili, "Dokta. Al-Bagoury," Mwalimu wa Uchumi katika Kitivo cha Mafunzo ya Juu ya Afrika, Chuo Kikuu cha Kairo, katika mfumo wa kozi ya mafunzo "Utangulizi wa Uchumi wa Afrika," alielezea matarajio ya Ajenda ya Afrika 2063. , Malengo madogo na mipango ya miaka kumi ya utekelezaji wake pamoja na  maelezo ya kina na mifano ya mipango iliyoanzishwa/iliyozinduliwa  na Umoja wa Afrika tangu kuzinduliwa kwa Ajenda mwaka 2013, pia ilishughulikia sifa kuu za uchumi wa Afrika, na changamoto za kiuchumi zinazokabili bara la Afrika, haswa wakati wa Janga la Covid-19. 


Ghazaly alihitimisha akiashiria  kuwa vyama vya wanafunzi ni miongoni mwa vyama muhimu vya vijana vinavyoweza kuchangia katika ujenzi wa taifa lenye nguvu, kufikia bara lililoungana, lenye nguvu ya kimataifa katika uwanja wa kimataifa, akisisitiza kuwa hilo ndilo lengo la mpango wa Afromedia kwa kuunga mkono taswira sahihi ya kiakili ya Bara la Afrika miongoni mwa  viongozi  wa vijana wenye ufanisi, ili kuongeza nafasi yao kama diplomasia ya vijana katika kuunga mkono uhusiano kati ya watu waarabu na Waafrika, kwa kufuata nyayo za uongozi wa Misri.

Comments