Majadiliano ya programu ya kitaifa " Mimi ni Mmisri .. Mimi ni Mwafrika" ili kuwafundisha wanafunzi katika mambo ya kiafrika
Kikao cha mazungumzo kinaongozwa na Mtafiti Menna Yasser Dessouki , miongoni mwa programu ya kitaifa "Mimi ni Mmisri .. Mimi ni Mwafrika " ili kuwafundisha wanafunzi katika mambo ya kiafrika , ambayo inapangwa na mpango wa Afromedia kwa ushirikiano na taasisi ya kiafrika ya kuendelea na kujenga uwezo , na baraza la ushauri la vijana kwa ajili ya makubaliano ya biashara ya huru ya kiafrika , na Shirikisho la wanafunzi wa kiafrika.
Dessouki alihitimu kutoka kwa Chuo Kikuu cha Ain Shams, Kitivo cha lugha , sehemu ya Lugha za kiafrika, Kiswahili , sasa yeye ni Mtafiti wa Uzamili katika Chuo Kikuu cha Kairo, Kitivo cha Masomo ya Kiafrika ya Juu , pia alihitimu programu ya waliojitolea katika Umoja wa Afrika .
Dessouki anafanya kazi kama Mfasiri wa lugha ya kiswahili huko ofisini mwa vijana wa kiafrika kwenye Wizara ya Vijana na Michezo , pamoja na kazi yake kama mtangazaji wa Redio mtandaoni kwa lugha mbili (Kiswahili na Kiarabu) , pia yeye ni mwalimu wa lugha ya kiswahili, na miongoni mwa ushiriki wake wa kiutamaduni ni kitabu cha NJIANI kwa lugha ya Kiswahili
Comments