"Kwanini Afrika?"

Mjadala wa jopo ndani ya programu ya kitaifa "Mimi ni Mmisri ... mimi ni Mwafrika" ili kujenga kada za wanafunzi katika masuala ya Afrika


Dokta. Nermeen Mohamed Tawfik, Mtafiti mhusika katika masomo ya kiafrika na masuala ya vuguvugu yenye msimamo mkali, na mratibu mkuu wa Kituo cha Ushauri na Masomo ya Kimkakati cha Pharos, anashiriki katika programu ya kitaifa "Mimi ni Mmisri ... mimi ni Mwafrika" ili kujenga kada za wanafunzi katika masuala ya Afrika, inayoandaliwa na mpango wa Afromedia kwa kushirikiana na Taasisi ya Maendeleo na Kujenga Uwezo ya Kiafrika, na Baraza la Ushauri la Vijana la makubaliano ya biashara huru ya Afrika, na Umoja wa Wanafunzi wa pamoja wa Afrika.


"Tawfik" alihitimu kutoka kwa Kitivo cha Vyombo vya Habari, Chuo Kikuu cha Kairo kwa daraja  nzuri sana kwa heshima, kisha akapata digrii za Uzamili na Uzamivu katika mifumo ya kisiasa ya Kiafrika kutoka Kitivo cha Mafunzo ya Juu Afrika, Chuo Kikuu cha Kairo, kisha akafanya kazi kwa miaka katika uwanja wa uandishi wa habari wa kielektroniki na utayarishaji wa programu, kisha akafanya kazi kama msaidizi wa mhariri mkuu wa jarida la masuala ya Afrika inayofuata Jumuiya ya Kisayansi ya Masuala ya Afrika ,na pia ni mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Jumuiya.


Katika kipindi kuanzia (2014-2018), Dokta. Nermeen Tawfik  alifanya kazi kama mhadhiri wa mfumo wa kuiga Umoja wa Afrika katika Chuo Kikuu cha Kairo, kisha kama mwalimu katika Taasisi ya Utafiti na Masomo ya Kimkakati kwa Nchi za Bonde la Mto Nile katika Chuo Kikuu cha Fayoum.


"Tawfik " amechangia katika uwanja wa masuala ya Afrika kwa vitabu na masomo  yaliyochapishwa katika magazeti na vituo vya kisayansi kwa kiwango cha kitaifa na kimataifa, labda maarufu zaidi kati yao ni: kitabu cha "Vuguvugu la Vijana Mujahidina Nchini Somalia na uhusiano wake wa kikundi cha Al-Qaida", na kitabu cha "Jeshi la Mungu la Upinzani nchini Uganda", licha ya ushiriki wake muhimu katika mikutano kadhaa na mahojiano ya televisheni.

Comments