Kwanini Afrika?!! .. Nermeen Tawfik ashiriki katika programu ya kitaifa; kujenga kada za wanafunzi katika masuala ya kiafrika
- 2022-02-11 00:06:04
Kwanini Afrika?!! .. Nermeen Tawfik ashiriki katika programu ya kitaifa; kujenga kada za wanafunzi katika masuala ya kiafrika
Mtafiti mhusika katika masomo ya kiafrika na mambo ya harakati zenye msimamo mkali, na mratibu mkuu wa kituo cha ushauri na masomo ya kimkakati cha Pharos Dkt, "Nermeen Tawfik" ameshiriki katika kikao cha majadiliano kinachoitwa "Kwanini Afrika?" ambacho ni sehemu ya programu ya kitaifa "Mimi ni Mmisri ...Mimi ni Mwafrika."; Ili kujenga kada za wanafunzi katika masuala ya kiafrika inayoandaliwa kwa mpango wa Afromedia kwa kushirikiana na taasisi ya maendeleo na kujenga uwezo wa kiafrika na baraza la ushauri la vijana la makubaliano ya biashara huru la Afrika na umoja wa wanafunzi wa pamoja wa Afrika kwa kushirikiana na jopo la viongozi wa vyama vya wanafunzi katika vyuo vikuu vyote kwenye Jamhuri, pia Mtafiti na mhitimu wa mpango wa kujitolea wa Umoja wa Afrika " Menna Yasser" ndiye aliyesimamia kikao hicho.
Tawfik aligusia maudhui muhimu kadhaa mnamo kikao cha majadiliano miongoni mwake ni Kuzungumzia umuhimu wa Afrika kwa mujibu wa ramani ya kijiosiasa ya ulimwengu, na pia kikao kiligusia matatizo makuu ya bara la Afrika mnamo wakati huu, haswa matatizo ya ugaidi na machafuko ya kisiasa, pamoja na kuonesha mifano ya miradi mikubwa ya maendeleo katika nchi kadhaa barani.
Katika muktadha huu, Tawfik aliashiria kuwa mchakato wa kurekebisha dhana na taswira ya kiakili kwa kada za wanafunzi wa vyuo vikuu vya Misri ni jambo muhimu sana sio tu kuwafahamisha historia ya pamoja kati ya nchi za kiafrika na sura ya Misri ya Kiafrika, lakini pia katika maendeleo makubwa yaliyoshuhudiwa kwa mahusiano ya Misri na Afrika katika kipindi cha hivi karibuni.
Mwanzilishi wa mpango wa Afromedia " Ghazaly" alihitimisha akionesha kazi ya mpango huo kupitia programu ya kitaifa ya kujenga kada za wanafunzi katika masuala ya kiafrika; ili kuunganisha utambulisho wa kitaifa na kuimarisha ujuzi wa tamaduni za kiafrika kwa kikundi hicho muhimu cha vituo vya vijana, kama mwanzo ili wachangie kwa jukumu lao kubwa katika kuelimisha wenzao kutoka vijana wa vyuo vikuu kwa lengo la kujenga mwamko wenye nguvu wa pamoja kwa umuhimu wa Umoja na Ushirikiano wa bara kwa vijana ambao wanachukuliwa kama viongozi wa siku za usoni.
Comments