Maha Jouini anashiriki katika mpango wa kitaifa wa kujenga kada za wanafunzi katika masuala ya kiafrika
Maha Jouini, Mtafiti mhusika katika Uwanja wa fani ya akili bandia na uchumi wa Afrika, anashiriki katika kikao cha “Mkataba wa Biashara Huria na Athari zake kwa Uchumi wa Afrika,” ambapo atajadili ufafanuzi wa makubaliano hayo pamoja na faida zake , mustakabali wake na athari zake katika ufufuo wa bara, ndani ya mfumo wa programu ya kitaifa "Mimi ni Mmisri ... mimi ni Mwafrika" ili kujenga kada za Wanafunzi katika masuala ya Kiafrika, iliyoandaliwa na Mpango wa Afromedia kwa ushirikiano na taasisi ya Afrika ya Maendeleo na Kujenga Uwezo, Baraza la Ushauri la Vijana kwa Makubaliano ya Biashara huria ya Afrika, na Umoja wa Wanafunzi wa Pan African, kwa kushirikisha viongozi wasomi wa vyama vya wanafunzi katika vyuo vikuu kwenye Jamhuri.
Maha Jouini aliteuliwa kuwa Mtu Bora wa Mwaka 2018 kwa jukumu lake kuu kama mshawishi kwenye mitandao ya kijamii, kulingana na jukwaa la Magharebia Voices.
Comments