Waziri wa Michezo akutana na wakuu wa mashirikisho mawili ya kimataifa na kiafrika kwa Mpira wa Kikapu
- 2022-02-13 11:06:52
Dokta Ashraf Sobhy Waziri wa Michezo na Vijana alikutana na Bwana Hamani Newong Mkuu wa Shirikisho la kimataifa kwa Mpira wa Kikapu na Bwana Anibal Mnaf Mkuu wa Shirikisho la Kiafrika kwa Mpira wa Kikapu na Bwana Amado Fal Mkuu a ubingwa wa mabingwa wa kiafrika , hiyo kwenye kando ya Ufunguzi wa Kombe la Dunia la Klabu la Mpira wa Kikapu linalifanyika kwenye Ukumbi wa Dokta Hassan Mostafa huko Oktoba 6 .
Mkutano huo ulizungumzia maandalizi na mipango ya kupokea tukio hilo la kimchezo la kimataifa ambalo ni Kombe la Dunia la Mpira wa Kikapu kwa ushiriki wa Klabu ya Zamale ya Kimisri inayowakilisha Bara La Kiafrika na klabu ya San Bablo Borgs ya Kihispania inayowakilisha Ulaya , na Flamengo kabu ya Kibrazil k
inayowakilisha Kusini ya Mrekani , na Lek Land Magice ya Kimarekani inayowakilisha Kaskazini mwa Marekani .
Waziri wa Michezo kupitia mkutano na Mkuu wa Shirikisho la Kimatiafa la Mpira wa Kikapu alisisitiza kuwa wizara ina nia ya kuvunja vikwazo vyote na kutoa nafasi ya uwezo unaosaidia katika mafanikio ya mashindano na matukio na shuhuli zote za kimataifa kama inavyofaa na umaarufu wa Kimataifa wa Misri, akiashria kwamba Misri inajua vizuri umuhimu wa Michezo na itaendelea kuwa mwiongoni mwa nguvu laini inayoweza kuwasanyika watu wote na kuondoa ubaguzi na vurugu na kukaribisha wananchi wa nchi tofauti .
Waziri huyo alisisitiza kwamba ushiriki wa Klabu ya Zamalek inayowakilisha Bara la Kiafrika , inaakisi uongozi wa Kimisri wa Kibara , akisifu uhodari wa Klabu ya Zamalek kupitia mechi yake ya nusu fainali ya ubingwa japo kutoshinda kwake , akiwaomba wachezaji wazingatie na wajitahidi ili kuhakikisha mafanikio ya medali ya Shaba ya Kombe la Dunia .
Dokta Ashraf Sobhy alisema kuwa uenyeji wa Misri wa Ubingwa huo unakuja ikiwa ni mwendelezo wa mfumo wa dola ya Misri kuandaa michezo na mashindano ya kimataifa kwa uungaji mkono kamili wa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri hiyo. msaada wote hutolewa kwa mashirikisho mbalimbali ya michezo ya Misri ili kutekeleza programu na mipango yao, na kushirikiana na mashirikisho ya kimataifa kuhusu upokeaji wa Misri wa mashindano yake mbalimbali.
Sobhy aliendelea, "Uongozi wa kisiasa wa Misri unatilia kujali kukubwa kwa michezo na unaona kuwa ni faili muhimu na kuu ya serikali ya Misri," akisisitiza kwamba Misri iko tayari kuandaa mashindano kutokana na uwezo na viungo vinavyoitambulisha Misri, na ukuaji wa ujenzi na mafanikio ambayo nchi inashuhudia chini ya uongozi wa Rais Abd El Fatah El-Sisi, ambaye hutoa msaada wote kwa mchezo wa Misri, ambao umepata mafanikio mengi katika kipindi cha kisasa.
Waziri wa Vijana na Michezo alidokeza kuwa mahudhurio makubwa ya wananchi kufuatilia mashindano ya michuano hiyo yanayofanyika kwa mara ya kwanza katika historia ya Bara la Afrika kwa mara ya kwanza yanaongeza msisimko na hamasa zaidi katika mashindano hayo, akieleza furaha yake kwa imani ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Kikapu baada ya kuipa Misri heshima ya kuandaa Kombe la Dunia la Klabu la Mpira wa Kikapu, ambalo litafanyika katika kipindi cha 11 hadi 14 Februari.
Wakati huo huo, Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Kikapu alithibitisha imani yake katika uwezo wa Misri wa kuandaa na kukaribisha mashindano hayo kwa kiwango cha juu, akiashiria ushirikiano wenye manufaa na mashirikisho ya Misri na Afrika kulenga kuwa na mashindano ya picha bora.
Comments