Waziri wa Michezo atafuta Maandalizi ya Misri ya kukaribisha mashindano ya Kombe la Dunia katika silaha ya Elshish
- 2022-02-13 11:07:47
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana michezo alikutana na
Bodi ya Wakurugenzi ya Shirikisho la Misri la silaha kwa uongozi wa Abd El Menem Al Hossiny ili kutafuta maandalizi ya Misri ya kukaribisha mashindano ya Kombe la Dunia katika silaha ya Elshish Na yatakayofanyika mnamo kipindi cha 25-27 Februari katika Kumbi zilizofunikwa kwenye uwanja wa Kairo wa kimataifa .
Mkutano ulijadili maandalizi yote yanayohusu mashindano , taratibu za Kumbi zilizofunikwa , vifaa na kila kitu kinachohusisha mechi , hoteli za kukaa , Makazi, taratibu za kuwasili kuanzia hoteli na viwanja vya michezo hadi kuondoka , utangazaji wa Runinga wa tukio hilo pamoja na hatua za tahadhari za wanaoshiriki katika mashindano ili Kuzuia virusi vya Corona kwa uratibu na Wizara ya Afya
Waziri huyo alisisitiza kwamba Misri kwa uongozi wa Rais Abd El-Fatah El Sisi ni msaidizi mkubwa zaidi wa michezo na mashindano ya kimataifa yanayofanyika ardhini na Dalili ni marekebisho ya ujenzi ya miundombinu ya kimichezo ya kimisri yaliyoifanya Misri isonge mbele Duniani kwa kufanya matukio , mashindano na shughuli za kimataifa
"Sobhy" aliongeza kwamba Wizara ya vijana na michezo inaunga mkono kwa mashirikisho yote ili kuratibu na kukaribisha mashindano mengi kwa kiwango kinachofaa jina la Misri na nafasi yake katika kuratibu mashindano katika
hali mbaya zaidi katika historia ya michezo wakati wa Janga la Corona.
Na kutoka upande wake , Bwana Abd El Menem El Hossiny, Mkuu wa Shirikisho la Misri la silaha alimshukuru Waziri wa vijana na michezo na Misri , akisifu juhudi za
Wizara za kutoa misaada katika viwango vyote na akiashiria msaada wa kimataifa wa mashirikisho yote ya mashindano yaliyoratibiwa na Misri mnamo kipindi cha mwisho .
"El Hossiny" aliashiria kwamba idadi ya nchi zilizosisitiza ushiriki ilifikia nchi 22 na wachezaji 101 na idadi imeamuliwa kufikia wachezaji 150.
Comments