Rais El -Sisi anaitembelea timu ya Misri kwa soka

Rais Abdel Fattah El-Sisi aliitembelea timu ya kitaifa kwa soka wakati wa mafunzo yake katika uwanja wa ulinzi wa hewa, kwa kuwepo Dokta Ashraf Sobhy,  Waziri wa Vijana na Michezo.

 

Balozi Bassam Radhi, Msemaji wa uraisi wa Jamhuri, alisema kuwa Rais Mheshimiwa  alikutana na wajumbe wa timu ya kitaifa ishirikiyo  katika  michuano ya Kombe la Mataifa ya kiafrika ijayo itayofanyika huko Misri na kuanzia Juni huu,  ambapo  mnamo  mkutano huo, Mheshimiwa huyo alionyesha matumaini yake halisi kwa Bahati nzuri na mafanikio kwa timu katika michuano, na aliwahakikishia kujiamini kwa wanachama wa chombo cha  kiufundi na wachezaji wa timu ya kitaifa  kwa jukumu waliyopewa, Na aliwaita wanachama wote wa timu kufanya jitihada kubwa ili kuwafurahisha  watu wa Misri,  ambayo inaonekana kwa heshima na shukrani..

 

pia Rais alisisitiza umuhimu wa wanachama wa timu wawe  na   nidhamu na tabia njema, Kuonyesha kuwa wao ni picha  ya ustaarabu na ukale  wa Misri , na inaonyesha thamani ya Misri na watu wake wakuu, na kukamilisha picha ya mwisho ya mafanikio ya michuano hiyo kwa utaratibu.

 

Msemaji huyo alielezea kuwa wachezaji wamemshukuru Rais kwa  heshima yake kwa kutembelea timu ya kitaifa kabla ya kushiriki katika michuano ya Mataifa ya kiafrika  , Wakimwahidi Mheshemiwa  Rais, kufanya jitihada za kuingia furaha kwa mioyo ya  mamilioni ya wamisri.

 

Balozi Bassam Radi aliongeza kuwa Mheshimiwa Rais Pia alifanya ziara  ya kichunguzi (alitangalia ) majengo na maandalizi ya uwanja wa ulinzi wa hewa ili kugusa mipango ya mwisho ya kuboresha  kwa uwanja huo ili kukaribisha mechi kadhaa za kombe la mataifa,  Rais alielezea matumaini yake kuwa michuano  hiyo itakuwa na nguvu nzuri kwa michezo ya kimisri kwa ujumla, na hasa kwa Soka, kutokana na maendeleo ya miundombinu ya michezo ya juu. 

Comments