Diplomasia maarufu katika mfumo wa mahusiano ya Afrika, fursa za ukamilifu wa kikanda na changamoto za ushirikiano wa pamoja
- 2022-02-13 11:11:58
Angelo William Jey , mhitimu wa programu ya wajitolea wa Umoja wa Afrika, anashiriki katika mpango wa programu ya kitaifa "Mimi ni Mmisri ... mimi ni Mwafrika" ili kujenga kada za wanafunzi katika masuala ya Afrika, inayoandaliwa na mpango wa Afromedia kwa kushirikiana na Taasisi ya Kiafrika ya Maendeleo na Kujenga Uwezo na Baraza la Ushauri la Vijana kwa Mkataba wa Biashara Huria wa Afrika, na Umoja wa Wanafunzi wa pamoja wa Afrika, kwa ushiriki wa viongozi wa wasomi wa vyama vya wanafunzi vya vyuo vikuu kwa kiwango cha Jamhuri, ambapo kikao kitashughulikia jukumu la Diplomasia maarufu katika mfumo wa mahusiano ya Afrika, licha ya kujadili fursa za ukamilifu wa kikanda na changamoto za ushirikiano wa pamoja.
Angelo William Jey alihitimu kutoka programu ya wajitolea wa Umoja wa Afrika mwaka wa 2017, alikuwa sehemu ya wajumbe wa Jamhuri ya Sudan Kusini katika Shule ya Kiangazi ya Afrika ya 2063, mwaka wa 2018, na sasa ni mtafiti wa shahada ya Uzamili katika sheria za kimataifa katika Chuo Kikuu cha Ain Shams, na ana shahada ya BSC katika sheria na Diploma ya mafunzo ya juu katika sheria za kibinafsi.
Jey ameshiriki katika shughuli kemkem pamoja na mashirika ya kimataifa, haswa: Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, shirika la Amani ya Kimataifa Bila Mipaka, na mamlaka ya Terre des Zooms ya Uswisi.
Hiyo licha ya Uanachama wa «Angelo William» katika mashirika kemkem ya jamii ya kiraia ya kitaifa na ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na: mjumbe wa ungamano wa Mazungumzo na Amani la Kiafrika nchini Morocco, pamoja na Uanachama wake katika ungamano wa Vijana la Afrika la Haki ya Mpito chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa, pamoja na Uanachama wake kama mwakilishi wa Jamhuri ya Sudan Kusini katika Muungano wa uvumbuzi wa kimataifa nchini Uhispania.
Comments