Waziri wa michezo ajadili maandalizi ya Misri ya kuifanya mikutano ya Shirika la kupambana dawa za kusisimua misuli kwa mara ya kwanza Barani Afrika


Waziri wa Vijana na Michezo Dkt, "Ashraf Sobhy" alijadili maandalizi na mipango yote ya Misri ya kuyafanya matukio ya mikutano ya baraza la uongozi na ofisi ya utendaji ya Shirika la kupambana  dawa za kusisimua misuli la kimataifa ( WADA) ambayo itafanyika mnamo Mei 2022, na inafanywa kwa mara ya kwanza Barani Afrika na eneo la mashariki ya kati kupitia mkutano alioufanya leo asubuhi na Shirika la kupambana Vichocheo la Misri ( NADO), Kwa mahudhurio ya mkuu wa Shirika la kupambana dawa za kusisimua misuli Misri, Dkt " Hazem Khamis" na mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo, Dkt " Hanem Alamir" na wawakilishi wa kampuni ya mipango ya Misri ya kuifanya mikutano, Na mkutano uligusia maudhui kadhaa miongoni mwake ni pande za kilojistea, teknolojia ya habari na programu ya kijamii kwa wenyeji na ujumbe wa Shirika.


Inapangwa kuwa Waziri wa vijana na michezo atafanya mkutano mkubwa wa uratibu mnamo Alhamisi ijayo na wawakilishi wa Shirika la kimataifa kupitia mkutano wa video; ili kujadili maandalizi ya Misri ya kuifanya mikutano ya WADA ya hivi karibuni na kujadili matakwa yote na Shirika la kupambana Vichocheo la kimataifa.


Ajenda ya mikutano ya baraza la uongozi na ofisi ya utendaji ya WADA  inajumuisha majadiliano ya maudhui kadhaa ya Shirika la kimataifa miongoni mwake ni mkakati wa kupambana dawa za kusisimua misuli wa kimataifa, hesabu za hitimisho, kamati za kudumu, kufanya mikutano na semina kwa mwaka mzima na kujadili udhibiti wa mashindano na taasisi za michezo, adhabu na hatua zinazotekelezwa Duniani.


Waziri huyo alisisitiza umuhimu wa upatikanaji wa uwezekano wote; ili kuhakikisha mafanikio ya tukio na kulitokea kwa namna inayofaa cheo cha jamhuri ya kiarabu ya Misri katika kufanya matukio na shughuli kadhaa za michezo ya kimataifa, kwa kuzingatia imani ya familia ya michezo ya kimataifa katika Misri na uwezo wake wa kiufundi, kilogestia na Uongozi.

Comments