Sambamba na Siku ya Wanawake katika uwanja wa Sayansi


"Maha Jouni" akizungumzia programu ya kitaifa ili Kuwajenga Kada za Wanafunzi katika Masuala ya Afrika 


Jouni, mtafiti mhusika katika uwanja wa akili bandia na uchumi wa Afrika, alishiriki katika programu ya kitaifa ya "Mimi ni Mmisri ... Mimi ni Mwafrika" ya kujenga kada za wanafunzi katika masuala ya Afrika, iliyoandaliwa na mpango wa  Afromedia Kwa ushirikiano na Taasisi  ya Kiafrika ya Maendeleo na Kujenga Uwezo, Baraza la Ushauri la Vijana la Mkataba wa Biashara Huria wa Afrika Na Umoja wa Wanafunzi wa Afrika Wote, kwa ushiriki wa viongozi wa wasomi wa vyama vya wanafunzi katika vyuo vikuu kwenye Jamhuri.

 Hivyo kupitia mjadala wa jopo kuhusu Mkataba wa Biashara Huria na athari zake kwa uchumi wa Afrika.


Katika kikao hicho, Jouini alijadili  masuala kadhaa, ambazo muhimu zaidi ni vikwazo  vinavyozuia kuharakisha uanzishaji wa Eneo la Biashara Huria la Afrika, pamoja na kushughulikia changamoto za nje zinazozuia ndoto hiyo ya bara, Mbali na kushughulikia jukumu la vijana kama nguvu  na diplomasia maarufu inayoweza kuathiri sana utashi wa kisiasa na watoa maamuzi ndani ya nchi za bara, mijadala hiyo pia ilishughulikia jukumu la mashirika ya kiraia katika kuamsha Mkataba wa Biashara Huria wa Afrika. 


Katika muktadha unaohusiana, Jouni aliashiria kuwa moja ya jukumu muhimu la vijana kwa sasa katika kuamsha Mkataba wa Biashara Huria Afrika ni kuhamasisha makundi yote ya jamii, Haswa wanawake, vijana na hata watoto kwa kuwa wao ndio tumaini la kesho na mustakabali wa bara letu, akisisitiza kuwa kuwajumuisha wanawake katika mifumo ya utekelezaji wa makubaliano hayo ni moja ya hatua muhimu zitakazochangia kwa haraka kasi kwa ujuzi na uungaji mkono kwa Mkataba wa Biashara Huria wa Afrika kati ya makundi ya kienyeji  Barani Afrika. 


Kwa upande wake, "Ghazaly" alisisitiza kuwa mpango wa Afromedia unahangaika kuunda mifumo ya kuhusisha kanuni za wanafunzi katika vyuo vikuu vya Misri katika utekelezaji wa makubaliano, kwa namna ya uongozi wa pamoja, Kulingana na mitazamo itakayowekwa nao wenyewe kwa ajili ya utaratibu wa kuamsha makubaliano hayo baada ya kuongeza ufahamu wao juu ya umuhimu wa Mkataba wa Biashara Huria wa Afrika na athari zake za kiuchumi haswa kwa Misri, na kuunda ushirikiano wa kiuchumi wa bara kwa ujumla. 

Comments