Waziri wa Vijana na Michezo ashiriki katika kikao cha “nafasi mpya kwa mustakabali” miongoni mwa shughuli za “wiki ya kiarabu ya maendeleo endelevu”


Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, Meneja wa Ofisi ya Mtendaji kwenye Baraza la Mawaziri wa Vijana na Michezo wa kiarabu, Jumanne Asubuhi alishiriki katika shughuli za “wiki ya kiarabu ya maendeleo endelevu” katika toleo lake la nne, iliyofanyika chini ya uangalizi wa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, kwa kichwa cha “pamoja kufikia nafuu  endelevu”.


Waziri huyo alizungumza na washiriki katika kikao cha “nafasi mpya kwa mustakabali” kinachojumuishwa na programu ya mkutano yaliyotengenezwa na Wizara ya Mipango na Maendeleo ya Uchumi kwa kushirikiana na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu mnamo kipindi cha 13-15 Februari hii.


Kikao hicho kilikuwa pamoja na Mahudhurio ya: “Dkt. Rasha Ragheb, Mkurugenzi mkuu wa Chuo cha Taifa cha Mafunzo ya Vijana,Bi. Maha Afifi, Mkurugenzi wa Mahusiano ya Serikali na Sera za Umma katika kampuni ya Google”.


Na katika maonesho yake, Waziri huyo alisisitizia shughuli za serikali ya Misri katika sekta zote, na kufanya juu chini kwa ajili ya maendeleo endelevu yanayozingatia taswira na mkakati wa kisayansi, pamoja na kuunganisha Misri pamoja na yote yanayotokea Duniani kote, na hivyo Chini ya usimamizi wa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, na uangalifu wake mkubwa kwa elimu na Utekelezaji, na kuweka Vipaumbele vya serikali ya Misri waziwazi kulingana na uadilifu, Uwazi na kutumia wataalamu na wenye uzoefu katika sekta mbalimbali.


Waziri aliongeza kuwa kuwajali Vijana kunakuja Mbele ya vipaumbele vya serikali ya Misri ambapo vijana wa Misri wakati wa kisasa wanashuhudia ujali wazi na usio na kifani, pamoja na kujali kwa mwanamke, na kutekeleza mkakati wa kuunda binadamu wa Misri kwa ajili ya kutekeleza maoni ya Misri.


Dkt. Ashraf Sobhy, katika hotuba yake, alizungumzia pia juhudi za Wizara ya Vijana na Michezo Kwa upande wa kuandaa viongozi wa vijana, na kuwawezesha, Ukuzaji wa Ujuzi wa Vijana, na kuongeza Utekelezaji wa programu na miradi iliyotekelezwa kwao ndani ya Taasisi za Vijana katika pande zote za Jamhuri miongoni mwa mwelekeo wa serikali kwenye uekelezaji wa binadamu, pamoja na programu za Wizara kwa upande wa maendeleo ya michezo na kugundua wenye vipaji na kuwajali.


Waziri huyo alisisitiza kuwa wiki ya kiarabu ya maendeleo endelevu inazingatiwa moja ya shughuli muhimu zinazoonesha maendeleo endelevu na juhudi zilizofanwa katika kazi ya maendeleo na mkutano wa wataalamu na wale wanaohusika na maendeleo endelevu, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa na kikanda na wawakilishi wa pande zote zinazohusika ili kuimarisha mazungumzo, majadiliano na kuweka mbele mipango ambayo itaimarisha juhudi za kupona baada ya Janga la Corona, akitoa shukrani na uthamini kwa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Wizara ya Upangaji kwa kuandaa mkutano huo, Akitarajia kutoa mapendekezo yanayofaa  yanayochangia kukuza maendeleo endelevu.

Comments