Chini ya kauli mbiu "Mazungumzo ya Bonde la Nile" ... Wizara ya Vijana na Michezo yazindua toleo la nne la Mradi wa Umoja wa Bonde la Nile...maoni ya baadaye


Chini ya ufadhili wa Waziri wa Vijana na Michezo, Dokta. Ashraf Sobhy, Wizara ya Vijana na Michezo, Utawala Mkuu wa Wachipukizi, Utawala Mkuu wa Watu Wenye Vipawa na Wabunifu, inajiandaa kuzindua Programu ya Mabalozi wa Mazungumzo ya Bonde la Nile. , ikiwa ni sehemu ya shughuli za toleo la nne la Mradi wa Umoja wa Nile ,Maoni ya Baadaye,  kwa ushirikiano na Mpango wa Afromedia wa vyombo vya habari  na mpango wa mabalozi wa mazungumzo, inayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 17 mpaka tarehe 21 mwezi huu ,Kairo. Hii inakuja ndani ya mfumo wa nia ya nchi ya Misri kuunga mkono na uhusiano wa pande mbili kati ya nchi za bara la Afrika, haswa nchi za Bonde la Mto Nile, katika jitihada za kuimarisha njia za mawasiliano na maelewano, na kuunga mkono na ushirikiano wa pamoja.


Mpango huo unalenga washiriki 150 kutoka nchi za Bonde la Mto Nile, Sudan, Misri na Jamhuri ya Sudan Kusini, katika kundi la umri wa kuanzia miaka 14 hadi 17, ili kuongeza uelewa kuhusu mambo ya pamoja kati ya nchi hizo tatu, kupitia kuwashirikisha katika mazungumzo kati yao wenyewe. , na kufafanua upya maoni yao kuhusu nafsi zao na wengine pia  bara la Afrika, na Dunia nzima, na kuimarisha uelewa wao wa thamani na utamaduni wa mazungumzo na athari zake katika kujenga Amani katika jamii.


Ni vyema kutambua kwamba Mradi wa Umoja wa Nile - Maoni ya Baadaye ni mradi wa mfumo uliozinduliwa mwaka 2017, kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa vijana kwa njia endelevu kati ya nchi za Misri, Sudan na Jamhuri ya Sudan Kusini, kupitia kufanya mikutano. na shughuli za vijana ambavyo vinakaribiana na  maoni na kuendeleza masuala yenye maslahi ya pamoja kama majadiliano ya vijana; kufikia mapendekezo yanayoweza kutekelezwa, huwasilishwa kwa mtoa maamuzi.

Comments