"Uhuru wa Maelekezo ya watu Barani Afrika"

Mjadala kwenye Mpango wa Kitaifa wa Kuandaa Kada za Wanafunzi katika Masuala ya Afrika

Dokta.Hamed Elmeslamy, Balozi wa Afrika Kaskazini katika Shirika la (AU_YAFTEMOPA) linalohusika na utekelezaji wa Itifaki ya Uhuru wa Kuelekea Watu Barani Afrika anashiriki katika mjadala ndani ya mpango wa kitaifa wa "Mimi ni Mmisri… Mimi ni Mwafrika" ili kuandaa kada za wanafunzi katika masuala ya Afrika ambayo imeandaliwa na mpango wa Afromedia  kwa ushirikiano na taasisi ya kiafrika ya maendeleo na kuimarisha uwezo

, baraza la ushauri la vijana la makubaliano ya biashara huria  ya kiafrika na  Umoja wa wanafunzi waafrika  kwa kushirikisha wasomi,

 viongozi wa vyama vya wanafunzi katika vyuo vikuu katika ngazi ya Jamhuri, na kikao hicho kitashughulikia suala la uhuru wa kuhama kwa watu binafsi katika Barani Afrika.


Elmeslamy alifanya kazi kama mtafiti katika Kituo cha Mafunzo ya Mashariki ya Kati - Paris katika ofisi ya kikanda huko Kairo, na alichapisha katika kituo hicho tafiti nyingi zinazohusika katika masuala ya Afrika, masuala ya Ugaidi na kuimarisha Amani na Usalama, pamoja na machapisho mengi. na utafiti wa kisayansi uliochapishwa katika majarida ya kisayansi katika lugha nne (Kiarabu , Kiingereza, Kifaransa na  Kijerumani).


Pia ni mwanachama mwanzilishi wa mashirika mengi ya kimataifa yanayohusika na masuala ya Afrika, mwanachama mwanzilishi wa Chama cha Mawasiliano cha Afrika katika Chuo Kikuu cha Kairo, pia mwanachama wa Chama cha Kisayansi cha Masuala ya Afrika, pamoja na kuwa mwanachama mwanzilishi wa Shirikisho la  (AU_YAFTEMOPA) kama Balozi wa Afrika Kaskazini, linalohusika na utekelezaji wa Itifaki ya Uhuru wa Kuhama kwa Watu Barani Afrika.


Elmeslamy pia alishiriki katika mikutano mingi ya kimataifa ndani na nje ya Misri, na katika mfumo wa uwakilishi wake kama Balozi wa mpango wa Umoja wa Afrika kwa Vijana kutoka kwa - Afrika Kaskazini - ili kutekeleza uhuru wa kuhama kwa watu binafsi Barani Afrika, alishiriki kama msemaji mkuu katika mkutano ulioandaliwa na Umoja wa Afrika nchini Nigeria ili kujadili Itifaki ya Uhuru wa Kuhama kwa Watu Barani Afrika, Lagos, Nigeria 2019, pia alishiriki katika mkutano wa Umoja wa Afrika, Mashirika ya Kikanda na Sekretarieti ya Mabunge ya Jumuiya za Kikanda za Kiafrika ili  kujadili Itifaki ya Uhuru wa Kuhama kwa Watu Barani Afrika huko Cotonou, Benin, 2021.


Elmeslamy alipata shahada ya Uzamili katika Sayansi za Siasa na masomo ya Kiafrika kutoka Kitivo cha Masomo ya Afrika ya juu kutoka Chuo Kikuu cha Kairo kuhusu “jukumu la Dini katika Maisha ya Kisiasa nchini Uganda.” Alishiriki katika kufundisha, kutoa mafunzo, kuandaa na kuratibu warsha katika matukio kadhaa katika vyuo vikuu vya Misri kwa wanafunzi wamisri na waafrika wasio wamisri.Sasa ni mtafiti wa Uzamivu katika Sayansi ya Siasa na Masomo ya Kiafrika, Kitivo cha Masomo ya Afrika ya juu , Chuo Kikuu cha Kairo, kuhusu jukumu la Mamlaka ya Utendaji katika uimarishaji wa Amani Barani Afrika.

Comments