Alhamisi ijayo .. Mpango wa "Afromedia" itazindua shughuli za kwanza za Mpango wa Mabalozi wa Mazungumzo ya Bonde la Nile kwa ushirikiano na Wizara ya Vijana na Michezo


Mpango wa "Afromedia" wa vyombo vya habari umetangaza, katika taarifa yake, leo, Jumanne, uzinduzi wa shughuli za kwanza za Mpango wa Mabalozi wa Mazungumzo na Bonde la Nile , Alhamisi ijayo, chini ya kauli mbiu "Misri yatuunganisha pamoja", ambayo imepangwa kufanyika kuanzia tarehe 17 hadi 21 Februari mwezi huu mjini Kairo, ikiwa ni mojawapo ya shughuli za Toleo la nne la Mradi wa Umoja wa Bonde la Nile "Maoni ya Baadaye ", ambao umeandaliwa kwa ushirikiano na Wizara ya Vijana na Michezo - Utawala Mkuu kwa Wachipukizi. 'i, na mpango wa Mabalozi wa Mazungumzo.


Mpango wa "Afromedia" wa vyombo vya habari umeongeza katika taarifa yake kuwa Programu ya Mabalozi wa Mazungumzo ya Bonde la Nile itahudhuriwa na washiriki 150 kutoka nchi za Bonde la Mto  wa Nile, Sudan, Misri na Jamhuri ya Sudan Kusini, katika kundi la umri wa kuanzia miaka 14 hadi 17. na ukiongeza kuwa upangaji wa mpango huo huonekana  wazi pamoja na utiliaji mkazo wa kudumu kwa serikali ya Misri  kwa kuunga mkono uhusiano wa pamoja  baina ya nchi za bara la Afrika, haswa nchi za Bonde la Mto Nile, pamoja na kufanya juu chini kwa lengo la kuimarisha njia za mawasiliano na maelewano, na kuunga mkono  ushirikiano wa pamoja kati ya nchi hizo tatu kupitia kuzishirikisha katika mazungumzo kati yao wenyewe, na kufafanua upya maoni yao kuhusu nafsi zao, wengine, na Bara la Afrika, pia Dunia nzima, pamoja na kuimarisha uelewano wao wa thamani na utamaduni wa mazungumzo na athari zake kwa  kueneza  Amani katika jamii.


Kwa upande wake, Hassan Ghazali, Mwanzilishi wa mpango wa "Afromedia" wa vyombo vya habari aliashiria kuwa uzinduzi wa mradi wa Kitengo cha Bonde la Nile " Maoni ya Baadaye" ulifanyika mwaka 2017 ukiwa ni mradi  uliozinduliwa kwa lengo la kuimarisha mahusiano kwa njia endelevu kati ya nchi za Misri, Sudan na Jamhuri ya Sudan Kusini kwa kufanya makongamano na matukio ya Vijana ambayo yangekaribisha  maoni na kufanya masuala yenye maslahi kwa pamoja kama majadiliano ili kufikia mapendekezo  yanayowezekana kuwasilishwa kwa watoa maamuzi.

Comments