Mjadala kwenye mpango wa kitaifa kujenga kada za wanafunzi katika masuala ya kiafrika. Dokta Mohammed Fouad Rashwan, mkuu wa mpango wa mafunzo ya kiafrika katika kituo cha RA cha mafunzo ya kimkakati.. ni mgeni wa mpango wa kitaifa {Mimi ni Mmisri... Mimi ni Mwafrika} kujenga kada za wanafunzi katika mambo ya kiafrika, ambapo anashiriki katika mjadala wa jopo kuhusu {Ushirikiano na Maendeleo Barani Afrika} .ambapo mpango wa Afromedia umepangwa kwa usharikiano wa Shirika la Maendeleo la Afrika na kujenga uwezo, na baraza la ushauri la vijana kwa mkataba ya biashara huria wa kiafrika , na umoja wa wanafunzi wa Afrika pamoja na ushiriki wa viongozi wa wasomi wa vyama vya wanafunzi katika ngazi za Jamhuri.
Mohamed Fouad Rashwan, mtafiti mhusika katika Masuala ya Afrika, ana Uzamivu wa falsafa katika masomo ya kiafrika kutoka idara ya Siasa na Uchumi, Kitivo cha mafunzo ya juu ya Afrika ,chuo kikuu cha Kairo kwa heshima za daraja la kwanza..
Dokta Rashwan ameongeza nyanja za masuala ya Afrika kwa fasihi na tafiti nyingi zilizochapishwa katika majarida ya kimataifa na pia kushiriki katika makongamano mengi ya kimataifa inayohusika mambo ya kiafrika ndani na nje ya Misri.
Dokta Rashwan alipewa kazi ya kufundisha katika taasisi ya mafunzo ya Bonde la Mto Nile katika chuo kikuu cha Fayoum katika idara ya Siasa na Sheria, hapo awali alifanya kazi kama msaidizi wa mhariri mkuu wa jarida la maduala ya Afrika,ni jarida la kisayansi linalirejelewa, katika kipindi cha 2013-2018..
katika mfumo wa ushiriki wake kama mwanachama mwazilishi katika kiungo cha mawasiliano ya Afrika, taasisi ya tafiti na mafunzo ya kiafrika..Dokta Rashwan alishiriki katika mafunzo na kupanga miundo ya Uigaji wa Umoja wa Afrika (AU) (mfumo wa kuiga Umoja wa Afrika 12 ) kwa usharikiano kati ya chuo kikuu cha Kairo, Wizara ya mambo ya nje ya Misri, Taasisi kuu ya Taarifa na ofisi ya Umoja wa Afrika mjini Kairo..
Dokta Rashwan anafanya kazi kama mhadhiri katika ofisi ya Umoja wa Afrika mjini Kairo katika kipindi cha 2015 hadi sasa mbali na kazi yake kama mhadhiri katika chuo cha Umoja cha mafunzo na Mashauri tangu 2010
Comments