Mabalozi wa mazungumzo ni mshiriki wa toleo la nne kwa mradi wa Umoja wa Bonde la Nile....... Maoni ya Baadaye chini ya kauli mbiu" mazungumzo ya Bonde la Nile"


Mradi wa mabalozi wa mazungumzo unajitayarisha ili kushiriki katika matukio wa toleo la nne kwa mradi wa Umoja wa Bonde La Nile.

Maoni ya Baadaye ,kwa ushiriki wa nchi za Bonde La Nile :- Misri , Sudan na Jamhuri ya Sudan kusini , katika kikundi cha umri kutoka miaka 14 hadi 17 kuongeza kwa ufahamu kuhusu mambo ya kawaida kati ya watu wa nchi hizo tatu , kwa kuwashirikisha katika mazungumzo yao wenyewe kwa wenyewe na kufafanua upya juu ya maoni yao kuhusu nafsi zao na wengine , bara la Afrika na Dunia nzima.


Mradi wa "Mabalozi wa mazungumzo " unafanya kazi ya kueneza utamaduni wa mazungumzo baina ya vijana tangu zaidi ya miaka kumi na mbili iliyopita kwa kushirikiana na baraza la vijana la Denmark. Ambapo mradi huo umezinduliwa tangu 2009 .

Katika mwaka wa 2017, Mradi huo nchini Misri  umechukua Mpango wa Misri- Danmark wa mazungumzo kama mwavuli wake.


Mradi wa " Mabalozi wa mazungumzo" unajumuisha zaidi ya wawezeshaji 200 wa mazungumzo kutoka mikoa mbali mbali ya Misri. Ambapo mradi unalenga kuwashirikisha vijana katika mazungumzo ya pamoja  na kufafanua upya maoni yao wenyewe , wengine na Dunia nzima.


Mradi  wa " Mabalozi wa mazungumzo "unatoa msaada wa kiufundi kwa washiriki kutoka taasisi ,mashirika ya kiraia na mipango

Msaada huo ni warsha ya mazungumzo kwa timu ya kazi na wajitolea kwa taasisi zao,

Warsha hizo zinafanya kazi ili kuinua ufanisi wa taasisi hiyo na kuifanya iwe kikamilifu zaidi na kutumia usawa, uaminifu na uwazi kama maadili ndani ya mazingira ya kazi.

Pamoja na kufanya warsha kwa walengwa wa taasisi zinahusu  mazungumzo ya binafsi na pamoja na wengine , wasaidie kufanya mazoezi ya mazungumzo katika maisha yao ya kibinafsi na kitaaluma pia kukubali Sheria ya Tofauti.

Comments