Mpango wa Afromedia ni mshiriki wa toleo la nne la Mradi wa Umoja wa Bonde la Nile ... Maoni ya Baadaye chini ya kauli mbiu "Bonde la Mto Nile"
- 2022-02-17 13:22:58
Mpango wa Afromedia unajiandaa kwa ajili ya ushiriki na utangazaji wa vyombo vya habari wa Mradi wa Umoja wa Bonde la Nile ... Maoni ya Baadaye katika toleo lake la nne chini ya kauli mbiu ya "mazungumzo ya Bonde la Nile", unaolenga kundi la vijana Wachipukizi kutoka umri wa miaka 14 hadi 17, kutoka wana wa Misri, Sudan na Jamhuri ya Sudan Kusini, ili kukamilisha jukumu lake husika la vyombo vya habari kama mpango mpya unalenga kubadilisha taswira mbaya ya kiakili kuelekea Afrika, kupitia kutoa mafunzo na kuelimisha makundi mbalimbali ya jamii, kwa kuinua uwezo na ujuzi wao kupitia kutoa mafunzo na ukarabati, katika maandalizi ya ushiriki wao katika maisha ya umma.
Vilevile mpango wa "Afromedia" unalenga kuwa daraja la vyombo vya habari kati ya watu wa Afrika, kupitia kuanzisha juhudi za maendeleo kuelekea bara la Afrika kwa wakati huu, kuangazia sura ya Afrika ya Misri, licha ya kuimarisha wajibu wa vyombo vya habari vya kisasa na jukumu lake la kuimarisha uhusiano kati ya Waarabu na Waafrika.
Pia katika muktadha huo, mpango wa Afromedia ulitoa programu kadhaa, matukio na paneli za majadiliano kwa vikundi tofauti vya jamii za kiafrika, haswa waandishi wa habari na wanataaluma wa vyombo vya habari, ili kuinua ufanisi wao na kusahihisha mtazamo wao kwa mambo ya bara, ukiuunga mkono kwa taswira sahihi ya kiakili ya bara la Afrika, na hiyo ndiyo lengo la uongozi wa Misri unalolitafutia.
Comments