Waziri wa Michezo awapongeza Ujumbe wa Misri kwa kushinda dhahabu ya wanawake na fedha ya wanaume katika mashindano ya Afrika ya mpira wa Vinyoya
- 2022-02-20 12:22:47
Dokta. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alipongeza Shirikisho la Misri la mpira wa Vinyoya kwa matokeo ya ujumbe wa timu ya Misri unaoshiriki ushindani wa mashindano ya Afrika ya mpira wa Vinyoya yaliyofanyika katika mji mkuu wa Uganda "Kampala" kuanzia 14 hadi 20 Februari hii.
Timu ya wanawake ya Misri iliishinda timu ya Uganda katika fainali ya mashindano ya Afrika kwa kiwango cha ushindani wa timu, ikapata dhahabu ya mashindano hayo, ilihali timu ya wanaume ilipata medali ya fedha katika ushindani wa timu, baada ya mechi yake pamoja na Algeria na kuchapwa katika Fainali ya mashindano hayo.
Waziri huyo alithamini utendaji, nafsi ya hali ya juu na juhudi zilizotolewa na wachezaji wa kiume na wachezaji wa kike wa timu ya taifa ya mpira wa Vinyoya katika mashindano ya Afrika, yaliyomalizika kwa ushindi katika ushindani wa timu kwa dhahabu ya wanawake na fedha ya wanaume, katika mafanikio mapya yatakayoongezwa kwenye rekodi ya mafanikio ya michezo ya Misri mwaka wa 2022, akitamani ujumbe huu kuendeleza ushindi na kushinda mashindano ya mmoja pekee yajayo.
Safari ya timu ya wanawake ya mpira wa Vinyoya katika mashindano ya Afrika kwa timu zote ilishuhudia kipaji cha hali ya juu, kwani wachezaji wa kike wa timu ya Misri waliweza kuongoza kundi lao lililojumuisha Algeria, Zimbabwe na Uganda na kuishinda Maurice katika hatua ya nusu Fainali hata wakifikia Fainali ya mashindano na kuishinda Uganda.
Ni vyema kutaja kuwa ujumbe wa Misri unaongozwa na Karim Shedid, Mjumbe wa Bodi ya Uongozi wa Shirikisho la Misri la mpira wa Vinyoya, na timu ya wanawake inajumuisha wachezaji wa kike: "Duha Hani, Nour Yousry, Hana Tarek, Jana Ashraf, Jana Hisham", na timu ya wanaume inajumuisha wachezaji wa kiume: "Ahmed Salah, Adham Hatem, Abdul Rahman Abdul Hakim, Muhammad Mustafa, Karim Mahmoud", na chini ya uongozi wa kiufundi wa kocha Mahmoud Ezzat na Abdul Rahman Kashakal.
Comments