Waziri wa Michezo aunga mkono Ujumbe wa Al-Ahly na Zamalek kabla ya ushiriki wao wa Afrika


Dokta .Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alikuwa na nia ya kupiga simu mara kadhaa na Balozi Hossam Issa, Balozi wa Misri nchini Sudan, na Bw. Al-Amri Farouk, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Al-Ahly, Mkuu wa Ujumbe,na Mashirikisho ya Soka ya Misri na Afrika; Kuangalia hali na mahitaji ya Ujumbe unaopatikana sasa nchini Sudan, na pia uratibu wa taratibu za kufanya mechi inayotarajiwa ya Klabu ya Al-Ahly na timu ya Al-Hilal ya Sudan katika Mashindano ya raundi ya pili ya kundi la kwanza katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, na Dk. Ashraf Sobhy, wakati wa simu zake, alitoa shukrani zake za dhati kwa wahusika wote Nchini Sudan na umakini wao kuhusu usalama wa ujumbe wa klabu ya Al-Ahly na kutoa mahitaji yote maalum ya ujumbe huo. 


Kwa upande mwingine, Wizara ya Vijana na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Usafiri wa Anga, ilikamilisha taratibu zote za safari ya ujumbe wa klabu ya Zamalek kwenda Angola kukabiliana na Sagrada Jumamosi ijayo katika mechi ya raundi ya pili ya Mechi za Makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. 


Waziri huyo alimpigia simu Waziri wa Usafiri wa Anga ili kumaliza tatizo la safari ya ujumbe wa Zamalek kwenda Angola, kutokana na taratibu za kiutawala na kifedha zinazohusu ndege binafsi ya ujumbe huo.


Waziri huyo aliweka wazi kuwa Wizara hiyo ina nia ya dhati ya kutatua matatizo yote zinazokwamisha ushiriki wa klabu zote za Misri katika mashindano ya bara na kimataifa, iwe ni kusafiri, au usalama wa Ujumbe wao nje ya Misri ili kuunda mazingira kwa wachezaji wetu kufikia mashindano na mafanikio Yanayowafurahisha mashabiki wa michezo wa Misri. 

Comments