Mpango wa "Afromedia" wa vyombo vya habari ulitangaza kuanzia ujio wa Washiriki wa Mpango wa Mabalozi wa Mazungumzo ya Bonde la Nile, Katika maandalizi ya kushiriki katika programu itakayofanyika ndani ya shughuli za toleo la nne la Mradi wa Umoja wa Bonde la Nile “Future Visions ( Maoni ya Baadaye )" chini ya kauli mbiu "Misri Yatujumuisha pamoja", Kwa ushirikiano na Wizara ya Vijana na Michezo - Utawala Mkuu wa Wachipukizi, na Mpango wa Mabalozi wa Mazungumzo, Imepangwa kufanyika kuanzia Februari 17 hadi 21, mjini Kairo.
Mpango wa "Afromedia" wa vyombo vya habari umeongeza katika taarifa yake kuwa hadi sasa, kikundi cha washiriki Wachipukizi kutoka nchi za Bonde la Nile "Sudan", Misri na Jamhuri ya Sudan Kusini, wameshafika katika makao makuu ya Mpango wa Mabalozi wa Mazungumzo ya Bonde la Nile katika Nyumba ya Mamlaka ya Uhandisi huko Kairo, na harakati hiyo inaendelea kupokea Washiriki wote wa mpango huo, ambao idadi yao ifikapo Wachipukizi 150 wenye umri wa kuanzia miaka 14 hadi 17.
Hassan Ghazali, Mwanzilishi wa mpango wa "Afromedia" ya vyombo vya habari, aliashiria Mahusiano ya kigeni ya Misri yameshuhudia ustawi mkubwa katika zama za Rais Abd El Fatah El-Sisi tangu ashike madarakani hadi sasa. Mahusiano ya Afrika, haswa pamoja na nchi za Bonde la Mto Nile na katikati yake kuna Bonde la Nile yanafurahia kwa umakini mkubwa kutoka kwa Nchi ya Misri, Akiongeza kuwa Utaratibu wa Mpango wa Mabalozi wa Mazungumzo ya Bonde la Nile, unaonesha wazi umakini wa mara kwa mara wa serikali ya Misri, Kusaidia mahusiano baina ya nchi za bara la Afrika, Haswa nchi za Bonde la Mto Nile, pamoja na kuhangaika kuimarisha njia za mawasiliano na maelewano, na kuunga mkono ushirikiano wa pamoja kati ya nchi hizo tatu kwa kuzishirikisha katika mazungumzo kati yao wenyewe, na kufafanua upya maoni yao kuhusu wao wenyewe, kuhusu wengine, kuhusu Bara la Afrika, na Dunia nzima, pamoja na kuimarisha uelewa wao wa thamani, na utamaduni wa mazungumzo, na athari zake katika ujenzi wa Amani katika jamii.
Seif El-Din Suleiman, Mhariri Mkuu wa Mtandao wa Vyombo vya Habari vya Sudazel na Mkuu wa ujumbe wa Sudan unaoshiriki katika Mpango wa Mabalozi wa Mazungumzo ya Bonde la Mto Nile, alithibitisha umuhimu wa mpango huo na jukumu lake katika kuboresha mfumo wa kijamii wa watu wa Bonde la Nile na kuinua uwezo wa watoto katika nyanja za uongozi na maendeleo endelevu, na kufungua upeo wa watoto hawa kuchangia vyema maendeleo ya nchi zao, Mbali na kuchangia muunganiko wa maoni katika maoni ya baadaye ya watu wa Bonde la Nile kupitia warsha na mihadhara iliyotolewa wakati wa programu.
Inafaa kuzingatia hilo kuwa Mpango wa mabalozi wa Mazungumzo ya Bonde la Nile utajumuisha mfululizo wa warsha, vikao vya mazungumzo, mijadala ya jopo, na michezo ya elimu na uhamasishaji, Shughuli za kwanza za programu zitaanza leo, Alhamisi, na kufahamiana kati ya washiriki, Pamoja na kuandaa warsha inayojumuisha uaminifu na shughuli za kujenga timu, pamoja na sherehe ya ufunguzi.
Comments