Wizara ya Vijana na Michezo yajadili "hatari za mitandao ya kijamii" ndani ya shughuli za mpango wa Mabalozi wa majadiliano ya Bonde la Nile


Wizara ya Vijana na Michezo chini ya usimamizi wa Dokta.Ashraf Sobhy  ilizindua shughuli za siku ya pili ya Mpango wa Mabalozi wa Majadiliano ya Bonde la  Nile, unaofanyika miongoni mwa 

sehemu ya shughuli za toleo la nne la Mradi wa Umoja wa Bonde la Nile. "Maoni ya Baadaye" chini ya kauli mbiu "Misri Yatujumuisha pamoja" na kikao cha mazungumzo 

 Chenye mada "Hatari za Mitandao ya Kijamii pamoja na Mahudhurio ya Dokta. Sayed Rashad, Mwalimu wa masomo ya lugha na Kiswahili katika sehemu ya lugha za kiafrika katika Kitivo cha Mafunzo ya Juu ya Kiafrika kwenye

Chuo Kikuu cha Kairo, pamoja na Mahudhurio ya mtafiti Yekwaj Vetter mtafiti wa sayansi za siasa na sekretarieti wa Masuala ya Elimu katika Kituo cha Urafiki wa Bonde la Nile  cha kielimu , na Mohamed Osama mtaalamu wa majukwaa ya mitandao ya kijamii.



Dk. Sayed Rashad Mwalimu wa masomo ya Lugha na Kiswahili katika sehemu ya Lugha za Kiafrika katika Kitivo cha Mafunzo ya Juu ya Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Kairo, wakati wa kauli yake alizungumzia hatari za mitandao ya kijamii,akiisifu kama kitu kingine chochote inawezekana kutumiwa, aidha chombo chanya au hasi, akieleza kuwa matatizo siku zote huja na huonekana kupitia matumizi hasi sio chanya, na anayetumia vyema mitandao ya kijamii katika kazi za kujenga, biashara, mawazo ya kibunifu, mawasiliano bora na wengine na kuchangamkia fursa hiyo ndiyo ni miongoni mwa matumizi chanya.


Mwanzoni mwa hotuba yake, mtafiti Yekoj Vetter, mtafiti wa sayansi za Siasa na sekretarieti wa Masuala ya Elimu katika Kituo cha Urafiki wa Bonde la Nile cha kielimu aliwasalimu washiriki wote na waandaaji wa Mpango wa Mabalozi wa Majadiliano ya Bonde la Nile pamoja na kutoa shukrani  kwa Wizara ya Vijana na Michezo kwa kuandaa programu hiyo muhimu kwa nchi za Bonde la Nile "Misri , Sudan na Sudan Kusini” na “Yekoj” alizungumzia jukumu la mitandao ya kijamii katika kushawishi nchi na watu na kuathiri tabia ya mtu binafsi na jamii kulingana na matarajio ya mtu binafsi au matarajio ya wengine.Pia alijadili majukumu hasi na chanya ya kutumia mitandao ya kijamii.


Naye Mtaalamu wa majukwaa ya mitandao ya kijamii Mohamed Osama aliongeza katika hotuba yake "Mitandao ya kijamii inapokea shime kubwa kutoka  kila mtu katika nyanja mbalimbali haswa katika nyanja za elimu katika kipindi cha hivi karibuni kutokana na athari za Corona na umuhimu wake mkubwa katika kufafanua kile kinachotokea na kinachozunguka  Duniani na katika nyanja za uchumi, biashara na shughuli mbalimbali, lakini chanya hizo hazikanushi hatari na hasi zinazotuzunguka kutokana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na yatokanayo na unyang'anyi, ulaghai,  na unyonyaji.

Alitoa maswali kadhaa kwa Washiriki wa Mpango wa Mabalozi wa Mazungumzo ya Bonde la Nile, kisha washiriki walipiga picha za ukumbusho huku kukiwa na mwingiliano, mapokezi makubwa na furaha kutoka  washiriki wote katika kikao hicho mashuhuri kuhusu hatari za mitandao ya kijamii.


Inafaa kuashiria kuwa uzinduzi wa Mradi wa Umoja wa Bonde la Nile "Maoni ya Baadaye" ulifanyika mwaka 2017 ikiwa ni mradi wa mfumo uliozinduliwa kwa lengo la kuimarisha uhusiano kwa njia endelevu kati ya nchi za Misri, Sudan na Jamhuri ya Sudan Kusini kwa kufanya mikutano na shughuli za vijana ambayo yataleta pamoja maoni na kuendeleza masuala yenye maslahi ya Pamoja  kwa majadiliano kama jukwaa linalotoa sauti ya vijana, matarajio yao na mapendekezo yao ya kushughulikia changamoto za maendeleo Barani Afrika .

Comments