Waziri wa Michezo asifu juhudi za Sudan ikifanikiwa kuandaa mechi wa Al-Ahly , Al-Hilal katika ligi ya mabingwa Afrika


Dokta. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na michezo alieleza Shukrani zake za dhati kwa Wizara ya Vijana na Michezo ya Sudan na Shirikisho la Sudan la mpira wa miguu kwa juhudi zao katika kuandaa mechi ya klabu ya Al-Ahly mbele ya timu ya klabu ya Al-Hilal ya Sudan uliofanyika jana nchini Sudan.


Mechi ya Al-Ahly na Alhilal ya Sudan ilimalizika kwa sare tasa katika mashindano ya raundi ya pili kwa kikundi cha kwanza katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika.


Waziri wa Michezo alithamini mafanikio ya kuandaa mechi hiyo katika nchi ndugu ya Sudan na mapokezi mazuri na kukaribishwa na watu ndugu wa Sudan kwa ujumbe wa Al-Ahly nchini Sudan, na hiyo ndiyo itakayofanyika tena kwa ujumbe wa Al-Hilal ya Sudan katika mechi yake mbele ya Al-Ahly huko Kairo akiashiria mahusiano mema ya ndugu na kihistoria yanayounganisha pande za Misri na Sudan.


Dokta . Ashraf Sobhy, alitamani Mafanikio kwa timu za Misri na ushindi katika mechi za ligi ya mabingwa Afrika ambapo Al-Ahly na Zamalek zinashiriki na michuano ya Shirikisho la Afrika pamoja na ushiriki wa Al Masry na Pyramids na kuendelea kupata mafanikio kwa kutwaa mataji yao, kusisitiza uongozi wa Misri katika Mpira wa Miguu Barani Afrika.

Comments