Waziri wa Michezo asifu mafanikio ya timu ya kitaifa ya Karate kwa Ukuu wa mashindano ya “Premier League” ikiwa na medali 9 tofauti*


 Waziri wa Vijana na Michezo Dokta Ashraf Sobhy alitathmini matokeo ya kipekee yaliyopatikana kwa timu ya kitaifa ya Karate wakati wa ushiriki wa michuano ya Ligi ya Dunia "Premier League" iliyofanyika Emirate ya Fujairah huko UAE mnamo kipindi hicho Februari 18-20. 


Waziri huyo alitoa pongezi kwa Shirikisho la Karate la Misri, na wachezaji wa timu ya kitaifa ya Karate kwa mafanikio yao katika Ligi Kuu, na kutwaa nafasi ya kwanza katika mashindano ya ubingwa kwa jumla ya medali 9, dhahabu 3, fedha 3 na shaba 3. 


Kwa hayo yote , timu ya Misri ilizishinda timu zote zilizoshiriki, na timu ya Kazakhstan ilishika nafasi ya pili kwa medali 4 mbalimbali, na Japan ilishika nafasi ya tatu kwa medali 5 mbalimbali.


 Wachezaji wa timu ya Karate ya Misri walifanya vyema wakati wa mashindano hayo, wakati ambapo Mchezaji wa timu hiyo Abdullah Abdel Aziz alishinda medali ya dhahabu katika mashindano ya kumite uzito wa kilo -75 wanaume, na Youssef Badawy alishinda medali ya dhahabu katika mashindano ya Uzani wa kilo -84 kwa wanaume ya Kumite, katika Fainali ya Misri kabisa ambapo Mohamed Ramadhani alishinda medali ya fedha. 


Na katika Uzani wa kilo +84, Hazem Muhamed alipata medali ya Dhahabu katika Fainali ya Misri kwa mara ya pili, pia Taha Muhamed alishika medali ya fedha.


Wakati mchezaji Yasmine Al-Juwaili akishinda medali ya fedha katika shindano la uzani wa kilo -50, mbele ya mchezaji wa Kazakh, na katika mashindano ya uzani ya kilo -55 ya wanawake ya Kumite, Ahlam Youssef aliweza kupata medali ya shaba. 


Feryal Ashraf alishinda medali ya shaba katika shindano  la uzani wa kilo -68, naye Ali Al-Sawy akashinda medali ya shaba katika shindano la Kumite la kilo -67 wanaume. 


Ikumbukwe kuwa timu ya kitaifa ya mchezo wa Karate ilishiriki mashindano ya michuano hiyo ikiwa na orodha ya wachezaji 17 wa kiume na wa kike, nao ni Malek Jumaa, Karim Mohamed, Ali Al-Sawy, Ahmed Lotfi, Hazem Saeed, Abdullah Mamdouh, Youssef Badawi, Taha Tariq. , Shahd Muhammad, Yasmine Al-Juwaili, Ahlam Hamdi, Faryal Ashraf, Norsin Muhammad, Menna Shaaban, Reem Ahmed, Aya Hisham na Habiba Maged, na timu hiyo iliongozwa kiufundi na Hani Kashta, kocha wa Kumite wa wanawake, pamoja na  Mohamed Abdel-Rahman, kocha wa Kumite wanaume, na Ahmed El-Sawy, Daktari wa ujumbe wa Timu,  ulioongozwa na Mohamed El-Dahrawi, Mkuu wa Shirikisho la Karate la Misri. 

Comments