Waziri wa Vijana wa Michezo ashuhudia kikao cha" Haki za Binadamu" ndani ya shughuli za mpango wa Umoja wa Bonde la Nile



Balozi  Mohamed Al Arabi na Balozi  Moshira Khatab ni wageni wa kikao cha mazungumzo.


Mkuu wa Baraza la kitaifa la Haki za Binadamu: Watu wa Bonde la Nile ni Watu wenye Amani, wanaunganishwa na Viungo vya pamoja, navyo vinatafutia Umoja, Tofauti, na  Heshima kwa Pamoja.


Waziri wa Hapo swali wa Mambo ya Nje: uhusiano kati ya watu wawili wa Misri na Sudan ni uhusiano Thabiti na, na Mpango wa Umoja wa Bonde la Nile ni ujumbe mzuri ili kuelimisha Wachipukizi na Vijana kwa viungo na mahusiano baina ya nchi hizo mbili.


Jumamosi,Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo alishuhudia kikao cha Majadiliano kilichofanyikwa kikiwa na "Haki za Binadamu" ndani ya Shughuli za Toleo la nne la Mpango wa Umoja wa Bonde la Nile"Mitazamo ya Baadaye" kwa kichwa cha " Majadiliano ya Bonde la Nile", unaotekelezwa na Wizara ya Vijana na Michezo mnamo kipindi cha tarehe 17- 21 Februari hii kwa ushiriki wa kikundi cha Wachipukizi kutoka Misri, Sudan na Sudan kusini.


kikao hicho cha Mazungumzo kilikuwa na  Balozi  Mohamed  Al Arabi, Waziri wa Hapo awali wa Mambo ya Nje na Balozi  Moshira khatab, Mkuu wa Baraza la kitaifa la Haki za Binadamu, na kuliongozwa na Mwanahabari Nshat Eldihi, na hivyo  pamoja na Mahudhurio ya Dokta Tarek Rahmi, Gavana wa Mkoa wa Gharbia, na Dokta Azza Aldary, Mkuu wa utawala mkuu wa Wachipukizi kwenye Wizara ya Vijana na Michezo, na Iman Othman Meneja mkuu wa idara ya wenye vipaji.


Wakati wa Kauli yake, Balozi Moshira khatab alisema: "Watu wa Bonde la Nile ni Watu wenye Amani wanaunganishwa na Viungo vya pamoja vya kihistoria, nasi pamoja tunatafutia Tofauti,Umoja, Ushirikiano,na  Heshima ya Pamoja Mbele ya Dunia nzima".

 

Aliongeza kwamba kuna kujali kukubwa kutoka kwa uongozi wa kisiasa wa Rais Abd El-Fatah El-Sisi katika kuimarisha mahusiano na nchi jirani, sio tu kwa upande wa nchi za Bonde la Nile, lakini nchi zote za Bara la Afrika na kutetea haki zao katika makongamano mbalimbali ambapo anashiriki.


Balozi Moshira Khatab alieleza juhudi za viongozi wa Afrika katika nyanja za uimarishaji wa Haki za Binadamu na kueneza Amani Barani Afrika na akiwemo kiongozi "Nelson Mandela" aliyezingatia kuunda Umoja wa kitaifa, kuunganisha nchi ya Afrika Kusini,  kutambua Utofauti na mazungumzo, na kuifanya Dunia nzima iangalie Afrika Kusini kupitia Michezo, Utamaduni na Ubunifu mbali na Vurugu, Chuki na Ubaguzi.


Wakati wa ushiriki wake, Balozi Mohamed Al Arabi alizungumzia uhusiano wake na nchi ya Sudan  ulioanza mnamo miaka ya Themanini, na maoni ya Misri na Sudan kama upanuzi wa Usalama wa kitaifa na kimkakati wa Misri, na ziara zake  mfululizo ndani ya mfumo wa mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili Misri na Sudan, akiashiria kwamba mpango wa Wizara ya Vijana na Michezo wa kuanzisha mkutano wa " Umoja wa Bonde la Nile.. maoni ya Baadaye" ni mpango muhimu wa kukuza umuhimu ya pamoja kati ya nchi mbili, na ujumbe mzuri wa Wizara kwa ajili ya kuelimisha Wachipukizi kwa viungo na mahusiano hayo baina ya nchi mbili.


Aliongeza :"Uhusiano kati ya Watu wa  Misri  na Sudan ni uhusiano thabiti, nasi sote tunapaswa kufanya juu chini ili kuimarisha mahusiano hayo kupitia matumizi ya njia mbalimbali katika kiwango cha viongozi, na mazungumzo pamoja na Watu wa nchi hizo mbili kama Wachipukizi na Vijana.


Washiriki walijadiliana kuhusu mambo kadhaa, ya muhimu zaidi ni viwango vya Utekelezaji wa  Haki za Binadamu, kuzipanua ndani ya nchi tofauti tofauti, pamoja na uwezo wa kuzihakikisha kwa wote na kuzingatia kufundisha Haki za Binadamu katika awamu mbalimbali za Elimu".


Balozi Moshira Khatab aliongeza kwamba Misri ni kutoka nchi zilizoshiriki kwa wanadiplomasia wa Misri katika kuandaa  Tangazo la kimataifa la Haki za Binadamu, ni kama Mama mkubwa aliyesababisha baadaye makubiliano ya Haki za Binadamu, pia aliashiria kuwa Tangazo la  Rais Abd El-Fatah El-Sisi, Septemba 2021 kuhusu Mkakati wa Haki za Binadamu kulingana na katiba ya Misri  inayohakikisha Haki za Binadamu kwa wote na utekelezaji wa makubaliano ya kimataifa yaliyochaguliwa na Misri, kwa hivyo Misri ikawa Duniani kama nguvu kubwa inazungumzia kwa lugha ya nchi za ulimwengu, kulingana na chaguo lake.


Balozi Mohamed Al Arabi na Balozi Moshira Khatab walieleza furaha yao kwa Ushiriki kikamilifu kwa washiriki wote katika Mkutano wa " Umoja wa Bonde la Nile" , na hali ya kuunganishwa na Ushirikiano kati ya washiriki, hiyo ndiyo inayosisitiza kufanikisha malengo yake, wakitoa Shukrani na kuthamini kwa Waziri wa Vijana na Michezo kwa kufanyika shughuli za mkutano, unaoshuhudia kikundi cha  vikao vya mazungumzo na warsha; ili kujadili mambo mbalimbali, kubadilishana maoni, mitazamo tofauti juu ya masilahi ya pamoja ya nchi hizo mbili.

Comments