Waziri wa Vijana ajadili kuimarisha ushirikiano na wawakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na UNICEF
- 2022-02-23 12:42:19
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alikutana na Fred Rika Meyer , Mwakilishi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu nchini Misri, na Jeremy Hopkins, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) ili kujadili kuimarisha ushirikiano wa pamoja katika kipindi kijacho.
Kikao hicho kilihusu maendeleo ya ushirikiano kati ya Wizara na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya Watu kupitia Klabu za Idadi ya Watu na Miradi ya Sanaa ya Jamii.Kikao hicho pia kilijadili taratibu za kuzindua mkakati wa Taifa wa Vijana na Wachipukizi ulioandaliwa na Wizara kwa ushirikiano Mfuko wa Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na
Taasisi ya Kiarabu ya kuwaandaa Viongozi kwenye Chuo cha Kiarabu cha Sayansi, Teknolojia na Usafiri wa Baharini.
Waziri huyo alithibitisha kwamba serikali ya Misri wakati wa enzi ya Rais Abd El Fatah El-Sisi ina nia ya ushiriki wa kijamii wa taasisi zote katika jamii ya Misri, na upanuzi wa kuimarisha ushirikiano na taasisi za kimataifa zinazounga mkono Vijana na Wachipukizi nchini Misri katika programu zao mbalimbali kwa kuzingatia nafasi ya kitaifa inayonufaisha jamii katika nyanja mbalimbali.
Sobhy alieleza Shukrani zake kubwa kwa pande hizo mbili kwa kuwepo kwao kukubwa na kwa bidii nchini Misri, na akisifu ushirikiano mzuri na wenye tija kati ya Wizara, UNICEF na Mfuko wa Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa katika programu mbalimbali zinazotekelezwa mnamo mwaka mzima.
Dk. Ashraf Sobhy alielekeza kufanya utafiti wa uanzishaji wa kitengo maalum cha klabu za watu zilizofikia 195, na pia akaelekeza upanuzi wa haraka wa uanzishaji wa klabu mpya katika vituo vya vijana kufikia klabu 400, ili kufikia mwendelezo na uendelevu katika ushirikiano kati ya Wizara na Mfuko pia aliagiza kufanya mfululizo wa mikutano na wawakilishi wa mashirika na programu za Umoja wa Mataifa ndani ya mfumo wa kuamsha mkakati wa kitaifa wa Misri kwa Vijana na Wachipukizi.
Waziri huyo alipitia na pande hizo mbili mradi wa Jukwaa la Vijana la Taifa “Kayani” na huduma zitakazotolewa kwa Vijana kupitia ushirikiano na ukamilifu pamoja na Wizara zote, akiwaalika kushiriki kikamilifu katika jukwaa hilo kwa upatikanaji wa haraka na ufanisi wa Vijana wa Misri.
Kwa upande wake, Fred Rika Meyer Mwakilishi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya Watu nchini Misri alisisitiza umuhimu wa ushiriki wa Mfuko huo na Wizara ya Vijana na Michezo huku akisifu maendeleo ya ajabu yanayoshuhudiwa na Wizara hiyo kwa kusaidia na kuwezesha vijana wengi waliofaulu mifano na mafanikio. akiishukuru Serikali ya Misri inayowakilishwa na Wizara kwa msaada wake wa kudumu na endelevu katika Mfuko huo.
Kwa upande wake Jeremy Hopkins, Mwakilishi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Watoto "UNICEF", alimwalika Waziri wa Vijana na Michezo kuhudhuria mkutano wa kilele wa vijana utakaofanyika chini ya kauli mbiu " kuanzia kujifunza hadi kupata kipato"
kwa ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika huko kwenye mji mkuu wa Jordan Amman Mei ijayo, akimshukuru Waziri wa Vijana kwa nia yake ya kuamsha ushirikiano na maagizo yake ya kupanua ili kufikia manufaa ya juu iwezekanavyo kwa vijana wa Misri kutokana na ushirikiano wa kimkakati pamoja na Mwakilishi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Watoto "UNICEF", linaloeleza uungaji mkono wa serikali ya Misri kwa shughuli za Mfuko huo nchini Misri.
Comments