Waziri wa Vijana na Michezo ashuhudia uzinduzi wa toleo la nne kwa Mpango wa Umoja wa Bonde la Nile
- 2022-02-23 12:47:14
Dokta.Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo alishuhudia uzinduzi wa matukio ya toleo la nne kwa Mpango wa Umoja wa Bonde la Nile " Maoni ya Baadaye", kwa kichwa cha " mazungumzo ya Bonde la Nile" Kwa ushiriki wa Wachipukizi wa Bonde la Nile. "Misri, Sudan ,Sudan Kusini" ambayo hufanyika katika kuanzia 17 kufikia 20 Februari 2022.
Na semina ya mazungumzo ilifanyika Kwa ushiriki wa Dokta.Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo , Balozi Al.sadik Omar Naibu ya Balozi wa Sudan, Balozi Jiprail Dinek, Balozi Mdogo wa Sudan Kusini, na Balozi Hany Salah Msaidizi wa Waziri wa mambo ya Nje wa Sudan ,
Mazungumzo yalisimamiwa na Ahmed Mokhtar, mhitimu wa kundi la pili la Udhamini wa Nasser Kwa Uongozi wa kimataifa.
Dokta.Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo akisisitiza Kwa kina ya mahusiano kati ya Misri na ndugu zake wote Barani Afrika haswa nchi za Bonde la Nile, kulingana na viungo kadhaa vinavyoziunganisha,
akieleza kwamba Nchi ya Misri ikiongozwa na Rais Abd El Fatah El Sisi inaelekea kuimarisha ushirikiano na mahusiano ya kidiplomasia pamoja na nchi tofauti.
Na akieleza kwamba mpango huo unalenga washiriki 150 kutoka nchi za Bonde la Nile " Sudan, Misri, na Jamhuri ya Sudan Kusini" katika umri baina ya 14 hadi 17,
ambapo unalenga kuongeza fahamu kati ya Vijana washiriki, na hiyo kupitia kuwajihusisha katika mazungumzo kati yao na kurudisha kufafanua maoni yao binafsi wao wenyewe, wengine,Bara la Afrika, na Dunia nzima,pia kuwaelewa thamani ya utamaduni wa mazungumzo na athari yake Kwa kuunda Amani katika jamii.
Waziri huyo aliongeza kwamba vikao hivyo hulenga kuboresha ustadi wao, uzoefu wao na kupanua mtazamo wao zaidi ya jamii zao na nyanja za ushawishi wao,kisha kuimarisha majukumu yao katika jamii, sio Kwa nchi yake tu,barani Afrika kikamilifu; kama maandalizi ya Uongozi wao Kwa mwendo wa maendeleo barani siku zijazo, akisema kwamba mpango uko katika toleo lake la nne, unasababishwa na Imani kubwa ya Wizara kwa umuhimu wa kuunganisha maadili ya mazungumzo na maelewano Kwa vijana, kwa lengo la kuwaandaa wawe viongozi wa siku za usoni.
Wakati Balozi Al.Sadk Omar, Naibu wa Balozi wa Sudan, akisisitiza kina ya mahusiano baina ya Misri na Sudan ,ambapo yana mizizi tangu zamani, akieleza kwamba vijana wanapaswa wawe na usimamizi mzuri wa wakati wao na kutumia kukuza ustadi wa kimwili na kiakili,linalosababisha Chanya kwake na kwa jamii, ili wawe nguzo muhimu wakiweza kuongoza jamii na nchi mnamo siku zijazo.
Na katika Kauli ya Balozi Jiprail Dinek Balozi Mdogo wa Sudan Kusini, akisisitiza umuhimu wa kuanzisha na kushirika katika mipango kama hiyo, akiongeza kwamba Vijana wanapaswa kupata faida kubwa zaidi kutoka mpango, wakati unashughulikia kupanua uwezo wa vijana na jinsi ya kuwasiliana na kuishi na wengine na kupata ujuzi mpya na uzoefu. Akieleza kwamba mpango huo katika toleo lake la nne una jukumu kubwa, hivyo unawataka vijana wote kufikia manufaa ya juu iwezekanavyo, watakuwa Mabalozi wa mpango katika nchi zao na kufanya kazi katika kuchapisha mawazo mazuri na kutupa mawazo mabaya.
Kwa upande wake, Balozi Hany Salah, Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje kwa Masuala ya Sudan, alieleza kufurahisha wake kuhudhuria mpango huo katika toleo lake la nne, akiongeza kuwa mipango kama hiyo iliyopitishwa na Wizara ya Vijana na Michezo ilikuwa sababu ya kumfanya sasa kama Msaidizi wa Mambo ya Nje ya Masuala ya Sudan, pia inaonesha ikiakisi shime kubwa ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kwa ndugu zao, na hiyo ndiyo iliyoonekana wazi katika Wizara ya Mambo ya Nje kulingana na Maelekezo ya Misri iliyoweka sehemu maalumu kuhusu Masuala ya Sudan na Sudan Kusini, linalothibitisha umuhimu wa uhusiano wa Misri na nchi hizo mbili.
Wizara ya Vijana na Michezo husimama mpango huo,kwa kushirikiana na mpango wa Mabalozi wa majadiliano , mpango wa Afromedia, na ushiriki wa Wachipukizi 150 katika umri wa miaka 14 hadi 17.
Ikumbukwe kuwa mwanzo wa mpango wa Umoja wa Bonde la Nile"Maoni ya Baadaye" ulikuwa mwaka 2017 kama mpango wa mfumo ulizunduliwa Kwa lengo la kuthibitisha mahusiano kwa maendeleo kikamilifu kati ya Misri, Sudan na Jamhuri ya Sudan Kusini,kupitia kufanyika Makongamano na shughuli za Vijana zenye lengo la kukaribisha maoni na kuweka Masuala ya kuvutia ya pamoja kwenye kama sehemu ya majadiliano kama jukwaa linaloeleza sauti ya Vijana, matakwa yao, na mapendekezo yao ya kukabiliana na changamoto za Maendeleo Barani Afrika.
Comments