Waziri wa Michezo pamoja na Vyanzo husika atafutia maandalizi ya mechi ya Misri na Senegal


Waziri wa Vijana na Michezo, Dokta Ashraf Sobhy alifanya mkutano wa kupangwa na kupanuliwa ili kujadili maandalizi yote yanayohusiana na mechi ijayo kati ya Timu ya kitaifa ya Misri na timu ya kitaifa ya Senegal Katika awamu ya mwisho ya kufikia Kombe la Dunia ، Mechi  iliyoratibiwa kufanyika Machi 25, 2022 kwenye Uwanja wa Kairo. 


Mkutano huo ulishuhudia kuwepo kwa wawakilishi wa taasisi mbalimbali za ulinzi na udhibiti, kampuni ya Tazkarti. Kampuni ya Afrika kwa Usalama, kampuni ya Presentation,  kampuni ya Astadant., na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uwanja wa Kairo. Na Shirikisho la Misri kwa Mpira wa Miguu. 


Na kwa upande wake, Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo alisisitiza kwamba Misri na taasisi zake zote zinaunga mkono timu yake ya kimisri , na zinashughulikia kushinda vikwazo vyote na kupatikana mahitaji ya michezo ya  kwenda na kurudi,

 haswa yaliyohusiana na kuwepo kukubwa kwa mashabiki  katika mechi ya kwenda katika  Uwanja wa Kimataifa wa Kairo ili kuunga mkono timu  kwenye Uwanja, Pamoja na msaada wa vyombo vya habari kwa timu yetu ya kitaifa.


 Akaongeza kwamba timu ya kimisri ilifanya vizuri katika michuano ya Afrika, na ilistahili kusifiwa na  Mheshimiwa Rais wa Jamhuri na kutoka kwa mashabiki wa michezo ya Misri ambao wanataka kushinda na kufikia Fainali za Kombe la Dunia.


Mikutano kadhaa imepangwa kufanyika mnamo siku zijazo kutangaza Wakati wa kupatikana Tiketi na  zitatolewa kwa bei kwa mashabiki kupitia Shirikisho la Soka la Misri,  “Mpira wa Miguu “, ambapo mashabiki 60,000 wameidhinishwa kuhudhuria mechi hiyo.


Waziri huyo wa Vijana na Michezo pia alisisitiza haja ya kuongeza kampeni za uendelezaji na vyombo vya habari ili kuwaomba mashabiki kuiunga mkono timu kabla ya mechi.


Na pia mkutano huo ulijumuisha majadiliano baadhi ya vidhibiti, haswa kwa kuingia kwa umma na kutoka na bima ya nje na ndani kwa viwanja vya mechi.

Comments