Waziri wa Michezo akutana na Bodi ya Usimamizi wa Shirikisho la kimisri kwa Sarakasi na kujadili kukaribisha Misri kwa Michuano ya Kombe la Dunia la Sarakasi
- 2022-02-24 23:24:55
Sobhy ….. Misri imekuwa mahali muhimu kwa michuano ya Dunia kwa sababu ya Uzoefu wake na msingi mwafaka.
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo alikutana na Dokta Ehab Amin Mkuu wa Shirikisho la kimisri na Mkuu wa Shirikisho la Afrika na Bodi ya Usimamizi wa Shirikisho la kimisri katika mfumo wa mfululizo wa mikutano ya Waziri na Bodi za Usimamizi wa michezo baada ya mwisho wa uchaguzi wa Mashirikisho.
Dokta Ashraf Sobhy ametoa pongezi kwa Bodi ya Usimamizi wa Shirikisho la Sarakasi baada ya kushinda Uchaguzi, akitakia bahati njema kwao katika kipindi kijacho, akaongeza kwamba michezo ya Sarakasi ilishuhudiwa maendelezo makubwa katika kucheza mnamo kipindi kilichopita.
Waziri huyo ameonesha hatua za kukaribisha Misri kwa Kombe la Dunia la Sarakasi iliyopangwa kuchezwa kupitia kipindi cha 15 hadi 21 Machi, 2022.
Waziri huyo ameeleza Furaha yake baada ya mafanikio ya Misri katika kukaribisha michuano ya kimataifa,
akisisitiza kwamba hiyo inaonesha mafanikio ya kimisri, ambapo ikawa mahali muhimu kulingana na Uzoefu mkubwa na kina yake katika kuanzisha na kuratibu michuano mikubwa ya kimataifa na Duniani.
Waziri huyo alisisitiza kwamba Shirikisho la kimisri la Sarakasi limefanya juhudi kubwa katika kushiriki michezo ya Sarakasi Nchini Misri na kupanuka fahamu ya mazoezi kwa Wote.
Mkutano huo pia umejadili mpango wa Shirikisho la kimisri kuwatayarisha mabingwa wa Olimpiki wawe wanaweza kushiriki na kushindana katika mzunguko ujao wa michezo ya Olimpiki.
Kwa upande wake Dokta Ehab Amin Mkuu wa Shirikisho la kimisri na kiafrika kwa Sarakasi alisifu Utaratibu na Ushirikiano kutoka upande wa Dokta Ashraf Sobhy na Wizara ya Vijana na Michezo katika kutoa kuunga mkono kikamilifu kwa Shirikisho la kimisri kwa Sarakasi.
Comments