Rasmi... Misri yaandaa mashindano ya Afrika kwa Baiskeli za barabarani mnamo Machi
- 2022-02-24 23:26:03
Shirikisho la Kimataifa la Baiskeli linaloongozwa na David Lappartian limeidhinisha uamuzi wa Shirikisho la Baiskeli barani Afrika kutoa rasmi kuandaa Mashindano ya Baiskeli barani Afrika kwa Misri, inayopangwa kuyafanyika mjini Sharm El-Sheikh kuanzia Machi 22 hadi 27.
Uamuzi wa kuandaa mashindano hayo nchini Misri ulikuja baada ya Burkina Faso iliomba radhi kwa Suala la kukaribisha mashindano hayo kutokana na hali za dharura.
Dokta. Wageeh Azzam, Mkuu wa Mashirikisho ya Baiskeli ya Misri na Afrika, na Makamu wa Mwenyekiti wa Shirikisho la Kimataifa na Kiarabu, alisisitiza kwamba kuandaa mashindano ya Afrika kwa Baiskeli ya Barabarani nchini Misri huonesha imani ya taasisi za michezo za kimataifa katika Misri, nchi ya Usalama na Amani, na uwezo wake uliothibitishwa wa kuandaa mashindano ya Barani na Duniani kwa mafanikio makubwa.
Dokta. Azzam alieleza kuwa Misri iko tayari kuwa mwenyeji wa mashindano hayo au tukio lolote la kimataifa la Baiskeli, kwa kuzingatia msaada mkubwa unaotolewa na Nchi ya Misri, Wizara ya Vijana na Michezo na taasisi zote za serikali kwa ajili ya kufanikisha kuandaa matukio makubwa ya michezo yanayoandaliwa huko Misri, linaloonekana wazi kupitia mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa mashindano mengi yaliyoandaliwa nchini Misri mnamo kipindi cha hivi karibuni Barani na Duniani.
Comments