Waziri wa Michezo ashuhudia mkutano wa kutangaza uenyeji wa Misri kwa michuano miwili ya Dunia ya mchezo wa El Shish na Upigaji risasi kwa Bunduki na Bastola
- 2022-02-28 11:38:56
Dokta Ashraf Sobhy : Misri ina Mali kubwa kwa upande wa ujenzi wa michezo na uzoefu wa kuandaa, ambapo ikawa kivutio cha kukaribisha michuano ya kimataifa.
Jumatano,Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alishuhudia, matukio ya mkutano wa waandishi wa habari uliofanyikwa kutangaza maelezo ya michuano ya Dunia wa mchezo wa Shish na michuano ya Dunia ya Upigaji risasi kwa Bunduki na Bastola kwa kuwepo kwa Meja Jenerali, Hazem Husni, Mkuu wa Shirikisho la Upigaji Risasi na Abdul Menem El_huseni, Mkuu wa Shirikisho la mchezo wa Silaha.
Michuano ya Dunia ya mchezo wa Shish ilipangwa kufanyika kuanzia Februari 25 hadi 27 kwa ushiriki wa wachezaji 183 kutoka nchi 33, ambapo michuano ya Dunia ya Upigaji risasi kwa Bunduki na Bastola inafanyikwa mnamo Februari 26 hadi Machi 8.
Dokta Ashraf Sobhy alithamini mafanikio ya mashirikisho mawili ya Upigaji risasi na El Shish kwa kiwango cha kuandaa michuano ya kimataifa, ushiriki mkubwa wa kimataifa wa wachezaji wamisri na kupanua msingi wa wachezaji wa michezo ya upigaji risasi na Silaha.
Waziri huyo alisisitiza kwamba Misri ikawa na utajiri mkubwa kwa upande wa ujenzi wa michezo na uzoefu wa kuandaa kwa michuano mbalimbali, matukio makubwa chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri, Abd El Fatah El_Sisi, pamoja na msaada wake wa kudumu kwa sekta za vijana na michezo, vilevile kuhimiza kuifanya Misri iwe kivutio cha mashirikisho ya kimataifa kukaribisha michuano yake mbalimbali.
Waziri huyo wa Michezo alibainisha kuwa Misri ilikaribisha michuano 138 ya kimataifa mnamo kipindi kilichopita, linalothibitisha uwezo wa Misri kuandaa na kuratibu matukio mbalimbali.
Mkuu wa Shirikisho la Upigaji Risasi alitoa shukurani na kumpongeza Waziri wa vijana na michezo juu ya kuunga mkono na kutia moyo kwake kila mara ili Misri ikaribishe michuano ya kimataifa ya Upigaji risasi, akionesha kwamba michuano ya Dunia ya Upigaji Risasi kwa Bunduki na Bastola ichukuliwe kama moja ya michezo mikubwa zaidi ya Upigaji Risasi, ambapo nchi 67 zinashiriki, akieleza kwamba Misri inaonekana kwa heshima Duniani wakati wa kuandaa michuano ya kimataifa, isitoshe umuhimu wa michuano ile kupanuka Utalii nchini Misri.
Mkuu wa Upigaji Risasi alibainisha Uenyeji wa Misri kwa Michuano minne ya kimataifa ya Upigaji Risasi katika mwaka huu, itaanza kwa mchuano wa Bunduki na Bastola Februari hii, mchuano wa kiafrika wa Upigaji Risasi utaanza Mei ijayo, mchuano wa Dunia wa Upigaji Risasi utaanza Oktoba ijayo, kombe la Rais, Novemba ijayo, akiashiria kuwa hiyo inakuja kwa kuzingatia imani ya Shirikisho la kimataifa la Upigaji Risasi kwa uwezo wa Misri ambayo imefikia mafanikio makubwa katika michuano ambayo imeandaa kipindi kilichopita.
Kwa upande wake, Mkuu wa Shirikisho la mchezo wa Silaha alisema:" michuano ya Dunia ya mchezo wa Silaha ya Shish inashuhudia ushiriki mkubwa katika ngazi ya idadi ya wachezaji na timu zinazoshiriki ikijiamini katika uwezo wa nchi kudhibiti uenyeji na uratibu", akionesha kwamba wachezaji wote bora hushiriki katika mchuano huu ambao uchukuliwe mchuano wa kwanza wa kufikia Olimpiki ya Paris 2024.
Aliweka wazi kwamba Uainishaji wa Misri, kwa sasa, unashika nafasi ya saba Duniani na Shirikisho la mchezo wa Silaha linachukua hatua za dhati kuboresha uainishaji wa kimataifa wa Misri kwa kupitia ushindi wa wachezaji katika mashindano mbalimbali wanayoyacheza, akitangaza uenyeji wa Misri kwa mchuano wa Dunia wa mchezo wa Silaha kwa wazima kwa mara ya kwanza Barani Afrika mnamo Julai ijayo.
Pembezoni mwa mkutano huo, Waziri wa Vijana na Michezo alishuhudia hafla ya kusainiwa kwa itifaki ya ushirikiano kati ya Shirikisho la mchezo wa Silaha na Mamlaka ya Posta ya Misri.
Comments