Wizara ya Vijana na Michezo “yazindua toleo la tatu la “Wiki ya Kiarabu-Kiafrika ya Kujitolea na Ujasiriamali” huko Sharm El-Sheikh
- 2022-02-28 11:41:15
Wizara ya Vijana na Michezo chini ya usimamizi wa Dk Ashraf Sobhy, inatoa toleo la tatu la “wiki ya kiarabu ya kiafrika ya kujitolea na Ujasiriamali,” kwa kushirikiana na Chama cha sauti ya Wanafunzi wa Misri, na hiyo wakati wa 24-28 Februari hii katika Jiji la Vijana huko Sharm El-Sheikh.
Hiyo inakuja wakati wa tangazo la Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El-Sisi la 2022 kama mwaka wa Jumuiya ya kiraia, na kulingana na maoni ya nchi ya Misri kuelekea kufikia maendeleo endelevu.
Wiki hiyo inajumuisha taasisi mbalimbali za Jumuiya, tawala, mipango ya vijana na makampuni yanayoibuka, zenye athari za kijamii katika ngazi za kitaifa, Kiarabu na barani Afrika.
Kuhusu vigezo vya kuchagua uwakilishi wa taasisi, mipango ya vijana na makampuni yanayoibuka, zenye athari za kijamii kushiriki katika shughuli za toleo la tatu la Wiki ya Kiarabu-Kiafrika ya Kujitolea na Ujasiriamali, ni kuwa zaidi ya miaka miwili imepita tangu kuanzishwa kwa taasisi au kipengee halisi tangu tarehe ya kuwasilisha, na makao makuu ya taasisi ya juu iko katika nchi za Kiarabu au za Kiafrika, pia taasisi hizo ziwe kimetekeleza au kukamilisha shughuli fulani katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, na kuwa malengo ya taasisi au tawala zinaendana na malengo ya maendeleo endelevu na Maoni ya Misri 2030, na tawala hizo zinajumuisha watu wa kujitolea au wafanyakazi kutoka mojawapo ya nchi za Kiarabu au Kiafrika.
Na taasisi iwe na shughuli katika mikoa zaidi ya moja katika ngazi ya Jamhuri, na taasisi inaunga mkono matumizi ya njia za kiteknolojia na mabadiliko ya kidijitali katika utekelezaji wa shughuli zake, na taasisi iwe na juhudi zinazohusiana na kukabiliana na changamoto za hali ya hewa kwa sasa kupitia shughuli zake mbalimbali.
Pia inahitajika kwamba mtu aliyeteuliwa kuwakilisha taasisi anapaswa kuwa na umri wa kati ya miaka 21-30 na awe mwanachama hai katika shughuli za tawala katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
Na wale wanaotaka kujiandikisha wanaweza kuingia kupitia kiungo https://forms.gle/kPeaW2Uq83SRwfnG6
Inajulikana kwamba Wiki ya Kiarabu-Kiafrika ya Kujitolea na Ujasiriamali – toleo la tatu.
Nao ni mradi ambao ulizinduliwa mwaka wa 2017 kama tukio maalumu la Misri ili kutoa mwanga juu ya athari za kijamii za taasisi, mipango ya vijana, watu wa kujitolea na watendaji katika kazi ya umma ili kuwaheshimu kwa jitihada zao katika jamii. Kufanya athari kuwa endelevu na kwa kiwango kikubwa kujumuisha watu wa kujitolea wa Afrika na nchi za Kiarabu.
Comments