Uzinduzi wa matukio ya toleo la tatu kutoka Wiki ya kiarabu ya kiafrika kwa Kujitolea na Ujasiriamali katika jiji la vijana huko Sharm El Sheikh


Shughuli za toleo la tatu kutoka Wiki ya kiarabu ya kiafrika kwa Kujitolea na Ujasiriamali zilizinduliwa katika jiji la vijana huko mji wa Sharm  El Sheikh ndani ya kipindi cha Februari  24 hadi  28  kushirikiana pamoja na jumuiya ya sauti ya vijana wa Misri.


Mkutano huo unakuja sambamba na maoni ya serikali ya Misri kuelekea kufikia Maendeleo endelevu.


Wiki ya kiarabu ya kiafrika kwa Kujitolea na Ujasiriamali inajumuisha taasisi za jamii, vyombo na mipango ya vijana na mashirika madogo  kuhusiana na athari za jamii juu ya kiwango cha kitaifa, kiarabu na kiafrika Taasisi Misri heri , jumuiya ya Resala , Taasisi ya Sonaa El Hayah ,Sanduku la kupambana Madawa ya kulevya, moyo mwekundu,hilali nyekundu, jumuiya ya El bar , I ber, Infenty ,Marofashion , Ofisi ya mawasiliano ya vijana, Shirikisho la kiarabu la Kujitolea,Baraza la makabila na familia za Misri, Jumuiya ya  nchi za kiarabu,familia kwa ajili ya Misri chuo kikuu cha Helwan, Chuo kikuu cha Misri cha Sayansi na Teknolojia, Baraza la vijana wa Misri, Taasisi ya vijana wa Misri kwa maendeleo 2030 Tuwalea vizuri, Misri kwa Vijana wake, Sauti ya vijana wa Misri, Thinking Academy.


Shughuli za leo zimeanzishwa kwa kikao cha ufunguzi, kwa kufafanua mkutano na onesho na kufafanua Ratiba ya matukio na kanuni pia kukaribisha Taasisi, Halafu kikao kuhusiana na mabadiliko ya kidijitali na uhusiano wake na Ujasiriamali ya kijamii, na zimehitimishwa kwa  matukio ya kugawanya vijana washiriki katika warsha za kazi kuhusiana na maudhui ya Kujitolea na kuunda Uwezo.


Ikumbukwe kuwa Wiki ya kiarabu ya kiafrika kwa Kujitolea na Ujasiriamali ni mradi ulioanzia mnamo 2017 kama tukio maalum la Misri kwa kuangazia athari ya jamii kwa taasisi na mipango ya vijana , wajitolea na wanaofanya kazi katika sekta ya umma kwa ajili ya kuwaheshima kwa juhudi zao katika jamii, pia  kwa ajili ya kuifanya athari hiyo iwe  endelevu na wigo mpana ikijumuisha wajitolea wa Afrika na nchi za kiarabu.

Comments