"Wizara ya Vijana na Michezo" yazindua Shughuli za kwanza za mkutano wa kwanza za utangulizi kwa Masoko ya kidijitali na kazi za mustakbali


Wizara ya Vijana na Michezo ikiongozwa na Dakta: Ashraf Sobhy , ilizindua mkutano wa kwanza kwa utangulizi wa Masoko ya kidijitali na kazi za mustakabali , kwa lengo la kuandaa vijana na ufahamu wao kwa mustakabali, pia jinsi ya kuwasiliana na Masoko ya kidijitali na hivyo ni wakati wa kipindi cha tarehe Februari 27 hadi Machi Mosi ijayo katika kituo cha Olimpiki huko Maadi.


Katika mkutano huo Wanafunzi kutoka Vitivo vya Teknolojia, Sayansi, Kompyuta katika vyuo vikuu vya umma vya Misri na vyuo vikuu vingine vya kibinafsi wanashiriki.

 matukio yameanza kwa mhadhara wenye kichwa: kuweka mkakati wa masoko (Masoko ya kidijitali)kwa mhandisi  Eman Wasfy, Mkufunzi katika Wizara ya Mawasiliano na Mshauri katika Benki ya kimataifa ambapo alitoa mwanga juu ya Masoko ya kidijitali na jinsi ya kushughulikia na kuzieleza bidhaa zao, pia njia ya kuvutia wateja na kurahisisha kuchagua bidhaa zao, ukifuatiliwa kwa mhadhara wenye kichwa "Usalama wa Habari na Usalama wa Akaunti"


Kwa Daktari: Hisham Afifi, Mshauri wa Usalama wa Habari na mabadiliko ya kidijitali, ambapo alidokeza umuhimu wa kasi katika mabadiliko ya kidijitali ya masoko na makampuni na kuzingatia Usalama wa Data na siri yake na umuhimu wa Usalama wa habari za kibinafsi na kulinda habari za fedha ,kazi , makampuni pia kulinda habari za Usalama wa kitaifa .

Comments