Waziri wa Michezo afuatilia siku ya mwisho ya mashindano ya Kombe la Dunia la Silaha ya El-Shish


Dokta. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, Jumapili, Februari 27, 2022, alishuhudia siku ya mwisho ya mashindano ya Kombe la Dunia la Silaha ya El-Shish katika Ukumbi namba1  katika kumbi  zinazofanikiwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Kairo, kwa mahudhurio ya Abd El Moneim Al Husseini, Rais wa Shirikisho la Misri na Naibu wa Rais wa Shirikisho la Kimataifa la mchezo huo, na vikundi vya Wajumbe wa baraza la uendeshaji wa Shirikisho hilo, Dokta. Abd El Awal Mohamed,Msaidizi wa  Waziri wa Vijana na Michezo, na Kafiro Givespi. , Mwangalizi wa Shirikisho la Kimataifa la Mashindano ya Kombe la Dunia la Silaha ya El-Shish.


Kuwepo kwa Waziri katika mashindano hayo kunatokana na msaada  wake na uungaji  mkono wake na kuhimiza pia kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Silaha wanaoshiriki mashindano hayo, na kuangalia maendeleo ya taratibu na mipango yote inayohusu mashindano hayo kwa kushirikiana na kamati ya maandalizi kwa mashindano hayo.


Waziri huyo alisisitiza ufuatiliaji wake  unaoendelea kwa  mashindano hayo, hadi yanapohitimu kwa sura inayolingana na jina na sifa ya Misri, na kubainisha  kuwa uwepo wa nchi 33 unasisitiza imani kubwa katika uwezo wa  Misri, na mafanikio yake katika kuchukua tahadhari zote za kujikinga na virusi vya Corona.


Mwangalizi huyo wa Shirikisho la Kimataifa alieleza kuridhishwa kwake na mpangilio mzuri wa mashindano hayo na kuchukua hatua zote za tahadhari katika Janga la Corona, akisisitiza juu ya uwezo wa Misri unaoiwezesha kuandaa mashindano yote ya Dunia kwa kiwango cha juu zaidi.


Al-Husseini alimshukuru Waziri wa Vijana na Michezo kwa uungaji mkono wake mkubwa kwa Shirikisho la Silaha la Misri na kuhimiza kwake kufanya mashindano ya Dunia nchini Misri.


Waziri wa Vijana na Michezo akifuatilia mchezo wa timu ya Misri dhidi ya  mwenzake wa Ufaransa katika mchezo wa kuainisha nafasi ya tano na sita, uliomalizika kwa kushindwa kwa timu ya Misri kwa mabao 45-38 na Misri inachukua nafasi ya sita kwenye mashindano hayo.


Timu ya Misri ilishinda Hong Kong 45-37 katika michezo za kuainisha nafasi kutoka tano hadi nane.


Timu yetu ya kitaifa iliishinda Canada katika raundi ya 16 kwa mabao 45-44, kisha ikashindwa na mwenzake wa Marekani katika robo Fainali kwa mabao 45-24.


Timu ya kitaifa inajumuisha miongoni mwa safu zake wachezaji 4, "Alaa Abu Al-Qasim - Muhammad Maher Hamza - Muhammad Hassan - Muhammad Essam".


Wafanyakazi wa kiufundi wa Mafarao ni: "Ashraf Massaad, kocha, Anas Mahmoud, kocha, Mustafa Nihad, kocha, Taha Youssef, Daktari wa timu, Ayman Ghoneim, mkurugenzi wa kiidara." Na Ahmed Nabil anasimamia timu za kitaifa. 


Comments