Waziri wa Michezo akutana na wafanyakazi wa kiufundi wa timu ya kitaifa kufuatilia maandalizi yake ya mechi za Senegal


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alifanya mkutano pamoja na Carlos kerosh, mkurugenzi wa kiufundi wa timu ya kwanza ya kitaifa ya Soka, na wanachama wa wafanyakazi wa kiufundi wanaomuunga mkono, Kupitia Video Conference.


Waziri huyo amehakikishia maandalizi yote ya wafanyakazi wa ufundi kuhusiana na mechi mbili za timu ya kitaifa dhidi ya timu ya Senegal ndani ya hatua ya mwisho ya kufikia  Fainali za Kombe la Dunia la FIFA 2022 nchini Qatar, pia  ufuatiliaji wa vifaa vya hali ya wachezaji wa timu ya kitaifa wnaopangwa kujumuishwa katika kambi ijayo ya mazoezi, pamoja na kujadili mahitaji  yote muhimu katika maandalizi ya mechi za Senegal.


Dokta Ashraf Sobhy alisisitiza uratibu na Shirikisho la Soka la Misri ili kupatikana mazingira yanayotakiwa na kuwa na hali kubwa ya kuzingatia ndani ya kambi ya timu katika maandalizi ya mechi za Senegal, akiashiria uungaji mkono na raia wa Misri kwa wachezaji wa timu ya kitaifa na wafanyakazi wa kiufundi kushinda jumla ya mechi mbili, nyumbani na nje , na kufikia mashindano ya Kombe la Dunia.


Katika muktadha unaohusiana na hilo, Dokta Ashraf Sobhy alikutana na Gamal Allam, Rais wa Shirikisho la Soka la Misri, ambapo walijadiliana  kuhusu maandalizi ya kuandaa Uwanja wa Kairo kwa ajili ya mechi ya timu ya kitaifa dhidi ya Senegal,  watazamaji wengi, na ratiba iliyowekwa ya mazoezi ya timu ndani ya kambi yake, iliyopangwa kwa siku zijazo, kwa uratibu na wafanyikazi wa kiufundi, na kutoa mahitaji yote.


Mchezo wa timu ya kitaifa dhidi ya Senegal utafanyika katika mkondo wa kwanza wa Fainali ya mwisho kwa Kombe la Dunia siku ya Ijumaa, Machi 25, katika Uwanja wa Kimataifa wa Kairo. Wakati mechi ya marudiano kati ya timu hizo mbili itafanyika Jumanne, Machi 29, katika uwanja wa Diamandio huko mji mkuu wa Senegal, "Dakar".

Comments