Msichana Msudan achukua mkondo mpya; kwa sababu ya mpango wa Wizara ya Vijana na Michezo


Miaka miwili iliyopita,Zeinab Mohi  El Din alikuja Misri, na maisha yake yalihusiana  kupata shahada ya chuo kikuu na kurudi kwa familia yake, akiwa Daktari; lakini Agosti 2021 mkondo wake ulibadilika, Na Msichana huyo wa Sudan alijiunga katika mpango wa wa mafunzo wa   " Meshwary" uliongozwa kwa Wizara ya Vijana na Michezo; ili kuendeleza ujuzi wa wanafunzi na wahitimu. 

Leo, Zeinab akawa mkufunzi wa watoto na ana jina la " Balozi wa mkoa wa Kairo" 


Zeinab alichaguliwa kuzungumzia uzoefu wake miongoni mwa makumi ya vijana walioshiriki mnamo siku ya Jumapili iliyopita katika sherehe iliyofanywa kwa makampuni makubwa ya bima ya Misri; ili kufanya protokoli mpya ya ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa wa kuhudumia watoto 

" UNICEF" ambalo ni mshiriki mkuu wa mpango wa " Meshwary" unaongozwa kwa Wizara ya Vijana na Michezo tangu mwaka wa 2008, kwa lengo la kuwawezesha Wachipukizi na Vijana kuanzia miaka 10 hadi 24 na kukuza ujuzi wao kupitia mipango ya kuendeleza uzoefu wa ubunifu wa mawazo, kuchukua maamuzi na Ujasiriamali na mpango huo ulitekelezwa katika mikoa 15. 


Zeinab alivumilia; kwa ajili ya ndoto yake, na ugeni ulimzidisha kwa matatizo yake na hisia za kukosa familia yake  " kwa kweli sikuona mama yangu tangu miaka minne; kwani anaishi nchini Saudi Arabia, na nilirudi Sudan kwa kusoma na nilikwenda Misri baada ya shule ya Sekondari" .


Ulimwengu ulimpungua, wakati alikuwa akitumia likizo ya nusu ya mwaka kwa muhula wake wa kwanza katika kitivo cha Tiba, alipatwa utupu.  " Bado masomo yalikuwa yataanza baada ya miezi miwili na sikuweza kusafiri, nilikasirika sana" .

Zeinab alitaka kile kinachomrahisisha siku, kwa hivyo alishiriki katika  mpango wa " Meshwary" ambayo mwenzake aliuweka kwa kundi la wanafunzi. 


Zeinab alivutiwa kwa tofauti kati ya mafunzo na utaratibu wa maisha yake, " Mwelekeo wangu wote ni wa kisayansi, wakati mpango ulikuwa unazungumzia stadi za maisha".  Msichana huyo hakutarajia mabadiliko yoyote kwenye maisha yake, alitaka tu kutumia wakati na kujaribu kuvunja mzunguko wa Upweke ulicho nacho.


Siku 5 katika kituo cha vijana cha  " Al_Basateen" zilifanya mabadiliko katika mkondo wa binti wa Sudan, " Haikuwa mihadhara ya kinadharia tu, bali chochote tutakachochukua kitakuwa na shughuli na nilipenda hivyo sana." 

Zeinab alirejesha uchangamfu na imani yake tena na mtazamo wake wa mambo,alipata ufunguo; kujaribu na kutatua matatizo yanayomkabili; lakini hali haikukomesha hapo. 


Baada ya muda Zeinab alirudi kwa mfumo wa maisha yake, hadi akashangaa, " Niliteuliwa ndani ya kikundi kilichochaguliwa kwa mpango na wakatupeleka kwa mafunzo ya pili; ili tukawa Mabalozi wa 

" Meshwary". Mpango huo uliendelezwa kutoka kujifunza ujuzi wa kibinafsi hadi kuchukua jukumu la kunakili wanachojua kwa watoto wenye umri wa miaka kati ya 10 hadi 14. 


Msichana mwenye umri wa miaka 21 alihisi kuwa amekuta njia ifaayo, na alifanya vyema katika mafunzo hadi alichaguliwa miongoni mwa watu 50; ili kuwafundisha watoto katika vituo vya Vijana. 


Kwa takriban miezi minne, tangu Novemba 2021, Zeinab amekuwa akisawazisha masomo yake katika chuo kikuu cha Helwan na kukutana na watoto wa wahamiaji na wakimbizi. Hatimaye, mwana wa Sudan alipata upole uliopoteza tangu alipokuja Misri. Msichana huyo alijua jinsi watoto hao wanavyohisi ugeni; kwa hivyo aliuwapa, akifuatana na maoni yao wakati wa siku za mafunzo, " Wote hawa ni marafiki, hakuna mtu anayehisi kuwa anatoka nchi tofauti, kuna watoto wanasema, Niliwafahamu marafiki wapya." Furaha ya watoto inaacha alama isiyoondolewa katika moyo wa Zeinab. 


Zeinab huwafundisha watoto juu ya fikira nzuri,kukubalika, mawasiliano na stadi nyingine za kibinafsi. Hucheza nao katika shughuli na kufuata mabadiliko yao katika siku zote za mafunzo, anawauliza katika siku ya kwanza kuhusu ndoto zao katika siku za usoni, anasikia majibu yanayorudisha " Nataka kuwa Daktari" na katika siku ya mwisho anarudia swali hilo na kupokea jibu kwa furaha ya pekee, " Kila mtoto ni wa pekee na anataka kuwa kile anachokipenda." 


Msichana huyo alidhani kuwa yeye peke yake ndiye aliyehisi mguso huo hadi alikabiliana na msimamo uliomzidisha furaha. 


Siku moja, alipokuwa akitembea katika eneo lake " Helwan", Mvulana mdogo aliyechukua mafunzo naye alimsimamisha na mamake alikuwa mara akamwambia " Mama,  Huyo ni mwalimu wangu", hali hiyo ilikuwa ndogo; lakini Zeinab alijivunia, " Ikiwa mwandamu alipata faida, nitakuwa kumpa kitu muhimu katika mwanadamu, na nilikuwa sababu ndogo kutoka furaha yake." 


Mwana wa Sudan alijua kwamba kile alichofanya hata ikiwa kidogo; lakini kitavuka mahali ambapo watoto hukutana. 


Katika miezi kadhaa, Maisha ya Zeinab yalibadilika, " Tamaa na maoni yangu yalikuwa madogo na niliona siku za usoni haiwezekani." 


Alitaka kuacha kila kitu; kusoma na kufanya mazoezi ya Tiba; lakini sasa anaendelea kutoa mafunzo kwa watoto na kushiriki katika mpango wa " Meshwary" anazungumzia uzoefu wake na anafurahia kwa ujumbe wa mama yake, ambaye alipokuta makala kuhusu elimu na mafunzo ya watoto, humtuma na kumtia moyo.


Zeinab akawa na imani kuwa milango mingi inamsubiri na ugeni wake haukuwa mbaya kama alivyofikiri. 


Comments